Vita vya kwenye Mto wa Feishui
中国国际广播电台


      Katika karne ya nne kulikuwa na madola mawili nchini China, moja ni Dola la Xianqin lililoko katika sehemu ya kaskazini, jingine ni Dola la Dongjin katika sehemu ya kusini. Mfalme wa Dola la Xianqin alitumia watu wenye elimu na washauri hodari, kuimarisha mamlaka yake na kustawisha kilimo, pamoja na hayo aliongeza nguvu zake za kijeshi akitumai kuliangamiza Dola la Dongjin.

Mwaka 383 mfalme wa Dola la Xianqin aliwaandikisha askari kutoka makabila mbalimbali hadi laki nane na elfu sabini. Kutokana na habari kwamba Dola la Dongjin wakati huo lilikuwa na askari laki moja tu.

Mfalme wa Dola la Dongjin alipopata habari kuwa jeshi la Dola la Xianqin lilielekea sehemu ya kusini kutaka kushambulia dola lake aliamuru askari elfu 80 kupambana nao, lakini wakati huo jeshi la Dola la Xianqin lilikuwa limekaribia mji mkuu wa Dola la Dongjin, hali ilikuwa ya hatari sana. Katika usiku wa siku moja majemadari wa Dola la Dongjin walishambulia kambi ya jeshi la Xianqin kwa kupanda farasi, walipata ushindi mkubwa, kisha wakaondoka haraka na kuficha askari wao kwenye mto wa Feishui, ambao ni mpaka kati ya Dola la Xianqin na Dola la Dongjin.

Mfalme walipopata habari kwamba askari wake waliotangulia walishindwa, kwa haraka alikwenda kwenye medani na kuwatia moyo askari wake. Aliposimama kwenye kilele na kuangalia upande wa pili wa mto aliona mehema mengi na bendera nyingi, hata aliona kila majani kama askari. Aliuliza wafuasi wake, “Dola la Donjin lina askari wengi, mbona mnasema halina nguvu?”

Mfalme wa Dola la Dongjin aliona kuwa ingawa askari wa Dola la Xianqin ni wengi, lakini walitoka katika makabila tofauti, hawana umoja. Zaidi ya hayo askari hao walisafiri sana kutoka kaskazini. Aliamua kumwandikia barua mfalme wa Dola la Xianqin na kumwambia awaachie nafasi ili askari wake wapite mto wa Feishui na kupambana na askari wake. Mfalme wa Dola la Xianqin alifikiri, atachukua fursa ya askari wa Dola la Dongjin kuvuka mto kuwashambulia. Lakini kinyume na alivyofikiri kuwa askari walipoambiwa warudi nyuma walifikiri askari wa mbele walishindwa, kwa hiyo walisambaratika. Kwa kutumia fursa hiyo jeshi la Dola la Dongjin lilifanya ushambulizi, askari wa Dola la Xianqin walikanyagana na wengi waliuawa, hata mfalme wa Xianqin alijeruhiwa.

Vita kwenye Mto wa Feishui, Dola la Dongjin lilishinda Dola la Xianqin lenye askari wengi kwa askari wachache.