Vita vya Chibi
中国国际广播电台


       Katika historia ya China vilitokea vita vingi ambavyo askari wachache waliwashinda askari wengi. Vita vya Chibi vilivyotokea katika Kipindi cha Madola Matatu ya Kifalme vinasimuliwa sana.

Katika karne ya pili, Enzi ya Han Mashariki ilikaribia kuporomoka, kutokana na vita kati ya majeshi, mwishowe walitokea majemadari watatu, Cao Cao, Liu Bei na Sun Chuan. Cao Cao alikalia sehemu ya kaskazini ya China, Liu Bei na Sun Chua walikalia sehemu ya kati na mashariki ya China. Mwaka 208 Cao Cao aliongoza askari wake kuelekea sehemu ya kusini kwa lengo la kumshambulia Liu Bei. Cao Cao alitamani kumshinda Liu Bei na kisha kumeza sehemu iliyokaliwa na Sun Chuan. Kutokana na hali hiyo, Liu Bei na Sun Chuan waliungana. Cao Cao aliongoza askari wake zaidi ya laki mbili na kukutana na askari elfu 50 wa Liu Bei na Sun Chuan kwenye sehemu ya Chibi. Askari wa Cao Cao walikuwa hawafahamu vita vya majini kwa sababu wote walikuwa ni askari wa nchi kavu, kwa hivyo, katika mapambano kadhaa jeshi la Cao Cao lilishindwa, alirudisha askari wake kwenye ukingo wa kaskazini. Majeshi ya Cao Cao na ya Sun Chuan na Liu Bei yalikabiliana kwenye kando mbili za mto. Baada ya kushindwa, Cao Cao aliamrisha mateka nyara wawili wa jeshi la Liu Bei na Sun Chuan kuwafundisha askari wake vita vya majini, na kweli walipata uzoefu. Kutokana na hali hiyo Sun Chuan alichochea fitina kati ya Cao Cao na maaofisa wake wawili waliotekwa nyara, kwamba hao wawili ni majasusi waliojificha ndani ya jeshi la Cao Cao. Cao Cao aliamini, akawaua maofisa hao wawili.

Majemadari wa Liu Bei na Sun Chuan walishauriana na jemadari Zhu Geliang namna ya kuwashinda askari wengi wa Cao Cao. Aliona kuwa kupambana na Cao Cao moja kwa moja kwa askari wachache hawatapata ushindi, aliamua kufanya mashambulizi kwa moto, alifanya mpango kamili. Kutokana na kuwa askari wa Cao Cao walikuwa hawajazoea vita majini, na waliona kizunguzungu walipokuwa katika mashua zilipokuwa zinayumbayumba. Wakati huo, mtaalamu mmoja wa mbinu za kivita, Pang Tong ambaye alimpendelea Sun Chun na Liu Bei alimwambia Cao Cao, “Hilo si tatizo, ukiunganisha mashua zote kwa mnyororo mashua hazitayumbayumba, askari watapigana kama wanavyopigana kwenye nchi kavu.” Cao Cao alifurahi sana kwa kupata ushauri huo. Lakini mshauri mmoja alisema, “lakini tukishambuliwa kwa moto tutakuwaje?” Cao Cao alicheka, “Usiwe na wasiwasi, musimu huu upepo unavuma kutoka kaskazini wala sio kutoka kusini.”

Lakini tarehe 20 Novemba mwaka 208 kwa kalenda ya Kichina, upepo ulivuma kutoka kusini, Zhu Geliang alikuwa na ujuzi wa kutabiri hali ya hewa. Kabla ya hapo kwa udanganyifu, jemadari wa Liu Bei na Sun Chuan walituma mtu kupeleka barua ya kusalimu amri katika siku hiyo. Cao Cao alisimama kijeuri juu ya mashua akiona kweli kuna mashua zaidi ya kumi zikimjia. Lakini mashua hizo zilipokuwa karibu na mashua za Cao Cao mara moto mkubwa uliwaka, kwa sababu ndani ya mashua walipakia mabua na mafuta, kutokana na kusukumwa kwa upepo wa kusini mashua hizo zikielekea kasi kwenye mashua za Cao Cao. Kutokana na mashua za Cao Cao zote ziliunganishwa pamoja kwa mnyororo, hazikuweza kuachana. Cao Cao alipanda ukingo, lakini ghala la chakula ukingoni pia liliwashwa na askari waliojificha huko. Cao Cao alitorokea sehemu yake ya kaskazini.

Baada ya vita vya Chibi utawala wa Sun Chuan katika sehemu ya kusini uliimarika, hali ya pande tatu ambazo kila upande haukuweza kuushinda upande mwingine iliendelea kwa miaka mingi.