中国国际广播电台
Liu
Bang ni mwanzilishi wa Enzi
ya Han Magharibi (206 K.K.—220).
Liu Ban alizaliwa katika
ukoo wa wakulima, mwanzoni
aliwahi kuwa ofisa mdogo katika
Enzi ya Qin, kwa sababu aliwaachia
wafungwa huru alitorokea mbali
na kujificha ili kukwepa adhabu
ya mfalme wa Qin. Mwaka 209
aliwakusanya wakulima wa maskani
yake kujiunga na jeshi la
uasi lililoongozwa na Chen
Sheng na Wu Guang. Baadaye
jeshi aliloongoza lilitangulia
kufika kwenye mji mkuu wa
Enzi ya Qin, Xianyang, na
kumaliza utawala wa Enzi ya
Qin. Katika mji mkuu wa Qin
alifuta sheria na kodi na
kuweka kanuni “aliyeua mtu
auliwe, aliyejeruhi mtu au
kuiba aadhibiwe”. Kutokana
na hayo alikaribishwa na raia.
Tokea hapo, Liu Bang alipambana
na jeshi la Xiang Yu kwa miaka
minne. Mwaka 202 jeshi la
Liu Bang lenye askari laki
tatu lilizunguka jeshi la
Xiang Yu, Xiang Yu alijiua,
Liu Bang alipata ushindi kamili
na katika mwaka 202 alikuwa
mwalme wa Enzi yake Han Magharibi.
Liu Bang alikuwa hodari
wa kuchagua wasaidizi wake
ambao mara nyingi walimsaidia
kusalimika katika hatari.
Hali iliyokuwa hatari kubwa
ni kushiriki kwenye karamu
ya Hong Men iliyoandaliwa
na Xiang Yu. Wakati huo jeshi
la Xiang Yu lilikuwa na nguvu
kubwa kuliko jeshi la Liu
Bang na Xiang Yu alitamani
kumwangamiza Liu Bang na kuwa
mfalme. Baada ya kufahamu
hali hiyo Liu Bang alikwenda
kwenye karamu akiwa pamoja
na mshauri wake Zhang Liang.
Kwenye karamu, jemadari wa
Xiang Yu alijitokea kwa kucheza
kitara kwa kisingizio cha
kuchangia furaha ya karamu
akitaka kumwua Liu Bang. Mshauri
Zhang Liang aliona hali ilikuwa
hatari, alimwamuru askari
kumlinda. Dakika chache baadaye
Liu Bang alitumia kisingizio
cha kwenda chooni alitoroka
na kurudi kwa siri. Kisha
mshauri wake aliingia kwenye
ukumbi wa karamu na kutoa
zawadi kwa Xiang Yu, na kumwambia
Xiang Yu kuwa Liu Bang keshaondoka.
Baadaye Liu Bang alikusanya
nguvu zake zote kulishinda
kabisa jeshi la Xiang Yu na
kuansisha Enzi ya Han Magharibi.
Baada ya kuwa mfalme, Liu
Bang alitunga sera nyingi
za kuendeleza uzalishaji.
Kutokana na vita vya miaka
mingi, idadi ya watu ilipungua,
aliwaachia wafungwa na watumwa
huru, aliwaachia askari wake
warudi nyumbani kushughulika
na kilimo.
Liu Bang alibeza wasomi,
aliona kuwa utawala wake ulipatikana
kwa vita, mashairi na vitabu
kwake vilikuwa havina maana.
Waziri wake Lu Jia alisema,
“Kitu kilichopatikana kutoka
mgongo wa farasi kinaweza
kutumika katika utawala?”
Kusikia hayo alimwagiza Lu
Jia aandike kitabu cha kueleza
sababu za enzi iliyotangulia
kushindwa ili kuboresha utawala
wake. Liu Bang alikaa madarakani
kwa miaka 12, katika mapambano
dhidi ya waasi alipigwa mshale,
baada ya kuugua muda alikufa.
|