中国国际广播电台
Miaka
4000 iliyopita mafuriko makubwa
yalitokea katika sehemu za
bonde la Mto Huanghe. Kutokana
na mchango wa kuondoa mafuriko,
Da Yu aliheshimiwa sana miongoni
mwa raia, mtemi wa kabila
la Wachina Shun alimwachia
nafasi yake. Hadithi kuhusu
Da Yu ilielezwa kizadi hadi
kizazi.
Inasemekana kwamba katika
miaka Yao alipokuwa madarakani
mafuriko yaliyokea, maji yaligharisha
mimea na nyumba, watemi wa
makabila yote walimchagua
baba wa Da Yu kwenda kupambana
na mafuriko. Baada ya miaka
tisa kupita mafuriko yaliendelea,
baba yake aliuawa kwa adhabu
na mtoto wake Da Yu aliagizwa
kupambana na mafuriko.
Da Yu hakufuata baba yake
alivyopambana na mafuriko,
bali alichimba mifereji na
kuyaongoza maji baharini.
Da Yu alifanya kazi sawa na
raia, kwa juhudi za miaka
13 mwishowe alifanikiwa kuyapeleka
mafuriko kwenye bahari.
Da Yu alianza kupambana
na mafuriko baada ya siku
chache kuoa. Siku moja alipopita
mbele ya nyumbani alisikia
kilio cha mtoto wake mchanga,
lakini hakuingia nyumbani
kutokana na shughuli.
Kutokana na mchango wake
mkubwa wa kuondoa mafuriko,
watu walimchagua kuwa kiongozi
wa muungano wa makabila.
Baadaye kabila la Da Yu
lilimpendekeza mtoto wa Da
Yu, aliyeitwa Qi, kurithi
kiti cha Da Yu, tokea hapo
utaratibu wa uchaguzi wa muungano
wa makabila ulifutwa na badala
yake utaratibu wa kurithisha
kiti cha ufalme ulitokea.
Enzi ya kwanza ya kifalme,
Xia, ilitokea katika mfumo
wa jamii ya utumwa nchini
China.
|