中国国际广播电台
Miaka
5000 iliyopita, Shen Nong
alikuwa mtemi wa kabila moja.
Katika zama za kale, mtemi
alikuwa sawa na watu wa kawaida
kufanya kazi mashambani, na
alipokuwa analima alivumbua
plau ambayo ilisaidia sana
kwenye maendeleo ya kilimo.
Kutokana na mchango wake huo
watu walimwita Shen Nong (mkulima
hodari).
Zama alipoishi Shen Nong
zilikuwa ni kipindi cha mwanzo
wa komuna ya ubaba, kulikuwa
hakuna unyonyaji wala ukandamizaji,
watu wote walikuwa sawa. Kutoka
na maandishi ya kale, katika
zama hizo wanaume walifanya
kazi shambani na wanawake
walifuma vitambaa, kulikuwa
hakuna gereza wala adhabu,
wala kulikuwa hakuna jeshi
wala polisi.
Shen Nong pia alikuwa mtaalamu
wa dawa wa mwanzo kabisa nchini
China. Inasemekana kwamba
aliona usumbufu sana alipoona
watu wanavyougua. Alifikiri
kwamba mazao yanaweza kusaidia
afya basi majani na mizizi
pengine inaweza kusaidia kuondoa
ugonjwa. Katika masimulizi
ya mapokeo, Shen Nong alichuma
aina mbalimbali za mimea na
kuonja, na alikuwa mara kwa
mara alipatwa na sumu. Aliwahi
kuandika kitabu cha “Dawa
za Mitishamba za Shen Nong”,
kikieleza maelezo ya tiba
ya magonjwa.
Kadhalika, Shen Nong pia
alikuwa mnajimu kwa ajili
ya kukumbuka mambo na kupiga
ramli. Zaidi ya hayo, alipoona
watu wanaolima mazao mengi
kuliko mahitaji, na baadhi
ya mazao wanayohitaji walikuwa
hawajui kulima, aliweka mahali
maalumu kwa ajili ya kubadilishana
mazao, hivyo kulitokea soko.
Shen Nong alikuwa madarakani
miaka 140, baadaye Huandi
alichukua nafasi yake. Alizikwa
katika mji wa Changsha wa
leo, mpaka sasa kuna kaburi
lake, watu wanaliita kaburi
lake kuwa kaburi la Yandi.
|