Hanfeizi
中国国际广播电台


Hanfeizi aliishi katika Enzi ya Vita vya Kivita (475 K.K.—221K.K.), alikuwa ni mwanafalsafa, na mwanasheria. Alikuwa wa kwanza kutoa nadharia ya kisheria kwa ajili ya utawala taifa wenye kiini kimoja.

Hanfeizi aliishi katika karne ya tatu ambapo ilikuwa ni kipindi cha mwisho cha Enzi ya Kivita. Alikuwa na kigugumizi, hakuwa hodari wa kusema, lakinialikuwa ni hodari wa kuandika vitabu.

Kitabu alichoandika “Hanfeizi” kilikusanya maandishi yote ya wanasheria wa Enzi ya Qin. Kitabu hicho kinachopatikana sasa kina makala 55 zenye maneno zaidi ya laki moja, na makala nyingi ni zake mwenyewe. Alitetea siasa ya kutoa zawadi kubwa kwa watu waliokuwa na mchango na kutoa adhabu kali kwa watu waliokuwa wahalifu, na kutilia maanani kilimo na nguvu za kupigana vita. Kadhalika alitetea kuwa madaraka ya mfalme yanawakilisha nia ya mungu. Tokea Enzi ya Qin yenye utawala wa kidikteta katika jamii ya kiumwinyi nadharia ya Hanfeizi ilikuwa na athari kubwa.