中国国际广播电台
Zhuangzi
aliishi katika karne ya nne
katika dola la Song, aliwahi
kuwa ofisa mdogo, alikuwa
mwenye akili na aliwahi kutembelea
kila mahali. Kutokana na werevu
wake aliwahi kualikwa na mfalme
wa Dola la Chu, lakini alikataa
na tokea hapo hakuwahi kuwa
ofisa, alijitenga na jamii
na kuishi kwa kusuka viatu
kwa majani. Inasemekana kwamba
aliandika vitabu vyenye maneno
zaidi ya laki moja.
Zhuangzi aliona kuwa maisha
ya binadamu lazima yawe ya
uhuru kabisa wala sio kuwa
na mali nyingi au sifa za
bure.
Pamoja na fikra za Zhouyi,
Laozi, fikra za Zhuangzi pia
zilikuwa athari kubwa katika
Enzi ya Tang (618—907).
Fikra za Zhuangzi hazielezwi
kwa nadharia tupu bali kwa
hekaya. Kitabu chake kilikuwa
kama ni mkusanyiko wa hekaya.
|