中国国际广播电台
Mencius
alikuwa ni mwanafikra mkubwa,
aliishi Enzi ya Madola ya
Kivita (karne ya 5 K.K. hadi
karne ya 3 K.K.) ni mmoja
wa wawakilishi wa fikra za
Confucius nchini China.
Mencius alirithi na kuendeleza
fikra za Confucius, alikuwa
ametofautisha wazi tabaka
la watawala na tabaka la watawaliwa,
alisema kuwa “wanaofanya kazi
kwa akili wanatawala, na waliofanya
kazi kwa nguvu za mwili wanatawaliwa”
na aliweka matabaka toka mfalme
hadi makabwera. Na wakati
huo alitetea kuwa uhusiano
kati ya watawala na watawaliwa
kama ni wazazi na watoto,
na kusema kwamba watawala
wawatendee vema raia kama
wazazi wao na raia wawatii
watawala kama wanavyowatii
wazazi wao.
Mencius aliunganisha nadharia
yake pamoja na siasa. Alisisitiza
kuwa maadili mema ni msingi
wa siasa. Alisema, “utawala
ni msingi wa taifa, na msingi
wa taifa ni familia, na msingi
wa familia ni maadili ya kila
mmoja.” Alisema kuwa kama
kila mmoja aliwatendea wengine
kwa maadili mema, utawala
wa kimnwinyi unahakikishwa.
Ili kufahamisha nadharia
yake alisema, asili ya binadamu
ni utu, aliona kuwa ingawa
kuna tofauti ya kazi na watu
wanaishi katika matabaka tofauti,
lakini utu ni mmoja.
Ingawa fikra za Mencius
zilikuwa na athari kubwa katika
historia ya China katika siasa,
fikra, utamaduni na maadili,
lakini haikuthaminiwa na mtawala
wa enzi yake.
|