中国国际广播电台
Zhang
Heng alizaliwa mkoani Henan,
alipokuwa mtoto alipenda sana
kujifunza na kuandika insha
na alipokuwa na miaka 17 alifika
mji wa Changan ambao uliwahi
kuwa mji mkuu wa enzi nyingi
katika historia ya China,
alipokuwa huko alifanya uchunguzi
wa kumbukumbu za kale, mila
na desturi za wenyeji na hali
ya uchumi ya jamii, kisha
baadaye alichaguliwa kuwa
ofisa katika mji wa Luoyang,
ambao ulikuwa mji mkuu katika
miaka yake. Lakini kutokana
na hamu yake na unajimu kwa
mara mbili aliacha kazi yake
ya ofisa na alitumia miaka
mitatu kufanya utafiti kuhusu
falsafa, hisabati, unajimu
na alipata elimu nyingi.
Katika miaka elfu mbili
iliyopita, elimu kuhusu ulimwengu
zilikuwa nyingi. Zhang He
aliona kuwa ulimwengu ni kama
yai, dunia ni kama kiini cha
yai, mbingu ni kubwa na dunia
ni ndogo, na aliona kuwa kabla
kutengana kwa mbingu na ardhi,
dunia ilikuwa ya mchanganyiko
wa vitu vyote, na baada ya
kutengana, vitu vyepesi vilipaa
juu na vitu vizito vilibaki
chini na kuwa dunia. Aliweza
kueleza mwendo tofauti wa
sayari kutokana na umbali
tofauti na jua, sayansi ya
zama hizi imethibitisha kuwa
mwendo wa sayari unahusika
na umbali na jua, kwa hiyo
mtazamo wa Zhang He ulikuwa
sawa.
Zhang He alibuni kifaa cha
kupima tetemeko la ardhi,
kifaa hicho ni cha mwanzo
kabisa duniani. Mwaka 138
kifaa hicho kilitoa habari
ya tetemeko la ardhi lililotokea
katika mkoa wa Shanxi.
Zhang Heng licha ya kuwa
mnajimu, naye pia alikuwa
mwanafasihi na mchoraji. Kutokana
na maandishi ya kale, Zhang
Heng alituachia maandishi
yake 32 kuhusu sayansi, falsafa
na fasihi. Na kati ya makala
hayo yako makala ya kueleza
msimamo wake wa siasa, kuna
makala inayoeleza matumaini
ya binadamu kusafiri katika
sayari nyingine na kuna makala
inayoeleza mandhari ya miji.
|