中国国际广播电台
Chen Sheng na Wu Guang walikuwa
ni viongozi mashuhuri wa uasi
wa wakulima, uasi ulioongozwa
nao ulikuwa mkubwa na wa kwanza
katika historia ya China ambao
ulizuka katika karne ya tatu
mwishoni mwa Enzi ya Qin.
Mwaka 210 mfalme wa kwanza
wa Enzi ya Qin alifariki,
mtoto wake Hu Hai alirithi
kiti cha ufalme.
Mfalme Hu Hai alikuwa mpumbavu,
chini ya utawala wake raia
waliishi vibaya na kutozwa
kodi nyingi.
Mwaka 209 mfalme Hu Hai aliamuru
wakulima 900 kwenda kulinda
mji wa Yu Yang (wilaya ya
Miyun karibu na Beijing).
Chen Sheng aliteuliwa kuwa
kiongozi wa wakulima hao.
Lakini walipokuwa njiani walizuiliwa
na mvua kubwa, walikuwa hawawezi
kufika mji wa Yu Yang kwa
wakati uliopangwa. Kutokana
sheria, wangechelewa wote
wangeuawa. Chen Sheng na Wu
Guang aliwaambia wakulima
kuwa ni afadhali kufanya uasi
kuliko kuuawa. Wakulima hao
waliwachagua Cheng Sheng kuwa
jemadari na Wu Guang kuwa
msaidizi wake na kuunda jeshi
la kwanza la wakulima katika
historia ya China.
Katika muda mfupi jeshi hilo
liliteka miji sita mikuu ya
wilaya na popote jeshi hilo
lilipopita raia waliliunga
mkono na kujiunga nalo. Jeshi
hilo lilikuwa na askari wengi
siku hadi siku na kuwa jeshi
kubwa lenye askari laki kadhaa.
Jeshi hilo liligawanyika
katika sehemu tatu, wakati
jeshi hilo lilipokuwa na askari
laki kadhaa walianza kushambulia
mji mkuu wa Enzi ya Qin.
Mfalme Hu Hai alishikwa na
hofu wakati jeshi la Cheng
Sheng na Wu Guang lilipokaribia
mji mkuu, alihamisha askari
laki kadhaa kuja mji mkuu
na kushirikiana na jeshi la
kifalme kupambana na jeshi
la uasi kutoka mbele na nyuma,
na Wu Guang aliuawa. Mwezi
Desemba mwaka 209 Cheng Sheng
pia aliuawa katika pambano
kali na jeshi la Enzi ya Qin.
Ingawa viongozi wa uasi huo
Chen Sheng na Wu Guang wate
waliuawa, lakini askari wao
walijiunga na jeshi jingine
lililoongozwa na Xiang Yu
na Liu Bang na kuendelea kupambana
na jeshi la Enzi ya Qin. Mwaka
206 Enzi ya Qin iliangushwa
na jeshi la uasi la wakulima.
|