中国国际广播电台
Kuna
hadithi moja kuhusu Su Wu
nchini China, nayo ni hadithi
ya “Mchugaji Kondoo Su Wu”.
Su Wu alikuwa mtu wa Enzi
ya Han katika karne ya kwanza.
Ili kuweka urafiki na kabila
la Waxiongnu lililoko katika
sehemu ya kaskazini magharibi
ya China Su Wu alitumwa na
mfalme kwenda kwa Waxiongnu
akiwa na zawadi nyingi, na
baada ya kumaliza kazi aliyopewa
na mfalme tayari kurudi nyumbani,
alibakizwa huko kwa kusingiziwa
kuwa alishiriki katika mgogoro
uliotokea ndani ya kabila
la hilo, na alilazimishwa
kuhaini Enzi ya Han.
Mwanzoni Su Wu alishawishiwa
kuwa ofisa kwa mshahara mkubwa,
lakini Su Wu alikataa, baadaye
aliadhibiwa na Xiongnu kwa
kutompa chakula na maji. Siku
zilikwenda, Su Wu alifungiwa
ndani ya shimo, akiwa na kiu
alikula theluji, akiwa na
njaa alikula koti lake ya
ngozi. Mwishowe aliachiwa
huru kutokana na nia yake
thabiti ya kutohaini Enzi
yake ya Han. Lakini hakuruhusiwa
kurudi nyumbani bali alifukuziwa
mbali kwenye sehemu ya baridi
Siberia kuchunga kondoo, aliambiwa
kuwa ataruhusiwa kurudi nyumbani
pindi kondoo dume akizaa.
Su Wu alifukuziwa kando ya
ziwa la Baikal na kuchunga
kondoo kwa miaka nenda miaka
rudi, nywele zikawa na mvi
na ndevu zikawa nyeupe.
Aliishi kwenye ziwa la Baikal
miaka 19. katika muda wa miaka
zaidi ya kumi mfalme aliyemfukuzia
alikufa, na mfalme wake wa
Enzi ya Han pia alifariki,
aliyeathiri kiti cha ufalme
alikuwa mtoto wake. Wakati
huo mfalme mpya alitekeleza
sera mpya na mfalme huyo mpya
alimtuma mtu kumrudisha Su
Wu nyumbani.
Su Wu alikaribishwa kwa shangwe
na wananchi katika mji mkuu
wa Enzi ya Han, maofisa wa
serikali walimheshimu kutokana
na uzalendo wake.
|