中国国际广播电台
Guan Zhong na Bao Shuya walikuwa
wanasiasa katika karne ya
saba na walikuwa marafiki.
Guan Zhong alikuwa maskini
na Bao Shuya alikuwa tajiri,
na hao wawili walifahamiana
na kuamiana na hata walishirikiana
kufanya biashara, kutokana
na umaskini Guan Zhong alitoa
raslimali chache, lakini walipogawana
faida alipewa pesa nyingi
zaidi kuliko Bao Shuya ili
aweze kuwatunza jamaa zake.
Baadaye watu hao wawili wote
walishiriki katika mambo ya
siasa, ambayo wote wawili
waliwafundisha watoto wawili
wa mfalme wa Dola la Qi katika
madola mengine tofauti. Baadaye
uasi ulitokea katika Dola
la Qi, mfalme aliuawa. Baada
ya kusikia habari kuhusu kifo
cha baba yao, watoto wote
wawili walikimbilia nyumbani
dola la Qi ili kurithi kiti
cha ufalme. Njiani mtoto Qi
Huan Gong na ndugu yake walikutana.
Guan Zhong alimfyatulia mshale
Qi Huan Gong ili ndugu wa
Qi Huan Gong apate nafasi
ya ufalme. Mshale huo ulimkwaruza
tu Qi Huan Gong kiunoni, lakini
alijidai kuwa amepigwa na
kuanguka kama amekufa. Ndugu
yake alidhani amekwisha kufa,
na kiti cha utawala hakika
kitakuwa chake, akapunguza
mwendo wa safari. Lakini Qi
Huan Gong hakuumia, aliharakisha
safari yake usiku na mchana
na alifika nchini mapema kwa
siku sita kuliko ndugu yake,
mawaziri walimwunga mkono
awe mtawala wa dola la Qi.
Baada ya kuwa mfalme wa dola
la Qi, Qi Huan Gong aliwapokea
watu wengi wenye busara hata
hakuwa na kinyongo na yule
Guan Zhong aliyemfyatulia
mshale na kumteua kuwa waziri
wa dola lake.
Guan Zhong alikuwa waziri
kwa miaka mingi na alitoa
mchango mkubwa kwa ajili ya
kuimarisha dola lake.
Bao Shuya alipofariki, Guan
Zhong alilia sana mbele ya
kaburi lake, alisema, “nilizaliwa
na mama yangu lakini aliyenielewa
ni Bao Shuya!”
|