中国国际广播电台
China ni nchi yenye uvumilivu
mkubwa, watu wanaona kuwa
uvumilivu unaweza kuyeyusha
fitina. Hadithi ya “kuondoa
kishungi kwenye kofia” inawafundisha
watu wenye uvumilivu watalipwa
mema.
Katika kipindi cha Spring
na Autumn, karne ya saba,
kulikuwa na madola mengi kwa
wakati mmoja. Mfalme wa Dola
la Chu, Chu Zhuangwang alikuwa
mwerevu, na chini ya utawala
wake dola hilo liliimarika
sana.
Siku moja, mfalme Chu Zhuangwang
aliwakaribisha maofisa kwenye
chakula na kuburudika kwa
nyimbo na ngoma. Giza lilikuwa
linaingia, mfalme aliwaambia
kuwasha mishumaa. Watu walikula
na kunywa kwa furaha.
Ghafla upepo ulivuma, mishumaa
ilizimika, wakati huo mke
wa mfalme alisikia kuna mkono
mmoja ulimshika shika, mke
wa mfalme alighadhabika akang’oa
kishungi cha kofia ya yule
aliyemtomasa, akaenda kwa
mfalme na kumnong’oneza, “washa
mishumaa na kuona kama nani
alikosa kishungi kwenye kufia
na kumwadhibu.” Lakini mfalme
alipaaza sauti na kusema,
“Msiwashe mishumaa, ni furaha
pekee kunywa pombe gizani.”
Baadaye mfalme aliwauliza
maofisa, “Mnafurahia chakula?”
wote walijibu “Ndio!” Mfalme
aliendelea, “kama kweli mnafurahia
chakula, basi ng’oeni vishungi
kwenye kofia zenu!” wote waling’oa.
Kisha mfalme aliwaambia wawashe
mishumaa. Maofisa walipoona
kofia zote zilibadilika sura
wote walicheka, waliendelea
kula na kunywa mpaka kupambazuka.
Baada ya kurudi kwenye kasri
la kifalme, mke wa mfalme
alihasirika sana alisema,
“Wewe mfalme unawadekeza sana
maofisa, hivyo utashindwa
kuwatawala.” Mfalme alicheka
na kusema, “Nawakaribisha
maofisa kwenye chakula kwa
lengo la kuwafurahisha. Ni
jambo la kawaida kwa mtu akizidiwa
na pombe na kufanya kitendo
kisicho cha kawaida. Nikimwadhibu
ofisa huyo kwa jambo hilo
dogo nitaharibu furaha na
kuwafedhehesha maofisa. Hilo
silo lengo la kuwaandalia
chakula.”
Baadaye dola la Chu lilishambulia
dola la Zheng. Kulikuwa na
jemadari mmoja aliyekuwa shupavu
mkubwa katika mapambano dhidi
ya askari wa dola la Chu,
na alifanya mashambulizi mpaka
karibu na mji mkuu wa dola
la Chu. Jemadari huyo ndiye
aliyemshikashika mke wa mfalme
wa dola la Chu.
Hadithi ya “kuondoa kishungi
kofiani” inawaambia watu wawe
wavumilivu.
|