Siku ya Tarehe 9 ya mwezi wa 9 kwa kalenda ya kilimo ya China yaani sikukuu ya Chongyang
中国国际广播电台

      Siku hiyo ni siku muhimu ya jadi ya China kwa wananchi wa China. Kila ifikapo siku hiyo, wachina wa familia moja moja wazee na watoto huenda kupanda milima na kuchuma matunda ya cornus na kula keki za maua waliotengeza wenyewe.

Wachina wa zama za kale waliona kuwa, tarakimu 9 ni ishara ya baraka, na tarehe 9 mwezi wa 9 ni siku inayoweza kuleta baraka mara dufu. Inasemekana kuwa, katika karne ya 3 kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, alikuwepo mtu mmoja aliyeitwa Fei Changfang, ambaye si kama tu alikuwa na uwezo wa kudhibiti upepo na mvua, pia aliweza kutuma malaika na kukamata mashetani. Kijana mmoja aliyeitwa Huan Jing alimheshimu sana Fei Changfang, alitaka kuwa mwanafunzi wake. Kutokana na nia yake imara, Fei Changfang alimchukua kuwa mwanafunzi wake, na kumfundisha mambo mbalimbali. Siku moja Fei Changfang alimwambia Huan Jing: “Tarehe 9 mwezi wa 9, familia yenu itakumbwa na msiba, kwa hiyo unapaswa kujiandaa kukabiliana na msiba huo.” Huan Jing aliposikia alihangaika sana, akapiga magoti mbele ya mwalimu wake akaomba amfundishe mbinu za kukwepa msiba. Fei Changfang alimwambia: “Siku hiyo ya tarehe 9 mwezi wa 9, ungeshona mikoba mingi myekundu na kuweka matunda ya cornus officinalis ndani, halafu weka kwenye mkono wako, uchukue pombe iliyowahi kutiwa maua ya chrysathemum , halafu watu wa familia yenu nzima muende kwenye mteremko wa mlima kunywa pombe, ndivyo hivyo mtakwepa msiba. Ilipofika tarehe 9 mwezi 9 kwa kalenda ya kilimo, Huan Jing na watu wa familia yake walikwenda kwenye mteremko kukaa na kunywa pombe kwa siku moja. Usiku waliporudi nyumbani kwao, waliona kuwa, mifugo waliyofuga nyumbani wote walikufa, kweli walikwepa balaa. Tangu hapo, kila ifikapo siku hiyo, wachina hupanda milima, kuchuma madunda ya cornus na kunywa pombe iliyowahi kutiwa maua ya chrysathemum , desturi hizo ziliendelea kwa zaidi ya miaka 2000.

Shairi moja lililoandikwa na mshairi maarufu sana wa Enzi ya Tang ya China ya kale Wang Wei lilionesha vilivyo desturi za sikukuu ya Chongyang. Shairi lake linasema: “Naishi nje ya maskani yangu, kila ifikapo sikukuu nawafikiria zaidi jamaa zangu. Naona ndugu zangu wote wakipanda mlima na kuchuma matunda ya cornus, nasikitika peke yangu niko nje na kuwakumbuka.”

Desturi nyingine ya sikukuu hiyo ni kula keki zilizotengenezwa kwa mchele, na tende, na kuweka bendera ndogo za rangi popote, hivyo keki hiyo iliitwa kuwa keki ya maua. Wakazi walioishi kwenye tambarare wakila keki hiyo, inamaanisha kuwa waliwahi kupanda milima, kwani keki ya kichina tamshi lake la kichina ni Gao, tamshi hilo ni sawasawa na tamshi la Gao nyingine yaani urefu wa mlima, hivyo watu wakila keki walijihisi kama waliwahi kupanda mlima.

Aidha sikukuu hiyo inoonesha maana ya “kuishi maisha marefu”. Kwani wachina waliona kuwa desturi za sikukuu hiyo zinaweza kuwawezesha watu waishi maisha marefu.

Hivi sasa wachina wanaendelea kudumisha desturia ya kupanda milima na kuchuma matunda ya cornus officinalis , hata dukani siku hiyo huuza keki za maua. Na miaka ya hivi karibuni, wachina waliona siku hiyo tarehe 9 mwezi wa 9, tamshi la 9 la kichina ni Jiu, tarehe 9 mwezi wa 9, kuna 9 mbili, tamshi lake ni sawasawa na neno la kichina Daima milele yaani Jiujiu, hivyo wachina waliamua siku hiyo kuwa ni siku ya wazee, maana ya sikukuu hiyo imeonesha wachina wanaoheshimu wazee, kuwapenda wazee na kuwatakia wazee waishi maisha marefu.