Siku ya Tarehe 5 mwezi wa 5 kwa kalenda ya kilimo yaani sikukuu ya Duanwu
中国国际广播电台

      Tarehe 5 mwezi Mei kwa kalenda ya kilimo ni sikukuu ya Duanwu, sikukuu hiyo na sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina pamoja na sikukuu ya Tarehe 15 mwezi wa 8 kwa kalenda ya kilimo ni sikukuu ya tatu muhimu kwa wachina.

Maana ya kichina ya “Duanwu” ni kuwa, “Duan” ni “Mwanzo”, kwa kufuata kanuni za kalenda ya kilimo ya kichina, tarehe 5 mwezi wa 5 ndiyo “Duanwu”.

Kuhusu chanzo cha sikukuu ya Duanwu, kuna ufafanuzi mwingi, baadhi ya watu wanaona kuwa sikukuu hiyo ilitokana na desturi za zama za kale za China, kila ifikapo majira ya siku za joto, na wengine walisema kuwa sikukuu hiyo inatokana na watu walioishi kwenye eneo la mtiririko wa Mto Changjiang walioabudu Dragong, lakini wachina wengi waliona kuwa sikukuu hiyo ilitokana na kumbukumbu za watu kwa mshairi mzalendo wa zama za kale Qu Yuan. Qu Yuan aliishi katika Dola la Chu katika karne ya 3 kabla ya Kristo, taifa lake liliposhambuliwa na maaduia kutoka nchi nyingine, alijitupa katika mto Guluojiang akiwa na huzuni kubwa, siku hiyo ilikuwa tarehe 5 mwezi wa 5 kwa kalenda ya kilimo ya kichina. Tangu hapo kila ifikapo siku hiyo, watu huchukua vyombo vya mianzi kuweka wali ndani na kuvitupa ndani ya mto kwa kumkumbuka Qu Yuan, baadaye wakatengeneza chakula cha Zongzi na kukitupa ndani ya mto.

Kula chakula cha Zongzi ni desturi muhimu katika sikukuu hiyo, Zongzi hutengenezwa kwa majani ya matete au majani ya mianzi, ndani huwekwa wali na hufungwa kwa nyuzi kuwa na umbo la sambusa, na kukichemsha hadi kiive. Kila ifikapo sikukuu hiyo, wachina hutengeneza chakula cha Zongzi na kukichukua kama zawadi kwa jamaa na marafiki.

Mbali ya Zongzi, katika sikukuu hiyo watu hula mayai ya bata yaliyowahi kutiwa chumvi na kunywa pombe ya kimanjano iliyotengenezwa kwa mchele, inasemekana kuwa kufanya hivyo watu wanaweza kukwepa mashetani.

Aidha, sikukuu hiyo pia kuwa desturia maalum ya kuchuma nyasi za wormwood kuzitundika kwenye mlango, nyasi hizo ni dawa ya mitishamba ambayo inaweza kufukuza wadudu wenye sumu. Kwani kila ifikapo sikukuu hiyo ya tarehe 5 mwezi wa 5 kwa kalenda ya kilimo yaani mwanzoni mwa majira ya siku za joto, mvua hunyesha sana, kuna kuwa unyevunyevu mwingi, na wadudu wenye sumu huzaliana wakati huo, ambapo ni rahisi kwa watu kupatwa na maradhi, na mitishamba hiyo inaweza kuwasaidia watu kukinga na kutibu maradhi. Na mpaka sasa, kila ifikapo sikukuu hiyo, wakazi wa vijijini wanashikilia desturi za kuwashonea watoto wao viatu vyenye sura kama chui, kwa maana ya kuwatakia watoto wao baraka.

Katika sehemu ya eneo la katikati na la chini la Mto Changjiang, kusini mwa China, desturi muhimu ni kufanya mashindano ya kupiga makasia kwenye mashua. Inasemekana kuwa desturi hiyo ilihusiana na wenyeji wa huko kumkumbuka mshairi mashuhuri Qu Yuan, wenyeji wa huko walipoona Qu Yuan amejitupa ndani ya mto, walipiga makasia mashua kwa haraka wakitaka kumwookoa. Baadaye kitendo hicho kilikuwa desturia ya kufanya mashindano ya kupiga makasia mashua.