Desturi za watu wa makabili madogomadogo ya China katika sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina
中国国际广播电台

      Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina ni sikukuu ya pamoja kwa watu wa makabila 56 wa China. Mbali na kabila la wahan, watu makabila mengi madogomadogo pia wanasherehekea sikukuu hiyo kwa desturi zao maalum.

Kabila la wa-li (wengi wanaishi mkoani Hainan, kusini ya China): wakati wa siku ya mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi, wa-li wa famili moja moja hukaa pamoja kunywa pombe na kula chakula, ambapo wanaimba nyimbo za kushangilia sikukuu. Tarehe 1 au 2 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo, walii huenda pamoja kwa uwindaji, na wanyama waliokamata, nusu kumpa mlenga shabaha wa kwanza, nusu nyingine kugawanywa kwa watu wote, kila mmoja atapata mgao mmoja, na mjamzito anaweza kupata migao miwili.

Kabila la wa-yi (wengi wanaishi mkoani Sichuan, kusini magharibi ya China): Wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina wayii hucheza ngoma kwa pamoja, ngoma hiyo unaitwa “Axi aruka kwenye mwezi” ili kusherehekea sikukuu. Katika baadhi ya vijiji, tarehe 1 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo, wanaume hufanya kazi za nyumbani na kuwaacha wanawake wapumzika siku hiyo, ili kuwapa pole kufanya kazi za nyumbani katika mwaka mmoja uliopita.

Kabila la wamiao (wengi wanaishi mikoani Hunan na Guizhou): wamiao huichukua sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina kuwa ni sikuuu ya “wakejia”, kila familia huchinja nguruwe na kondoo, kuombea mvua na mavuno. Aidha wamiao huimba wimbo wa “Mwanzo wa siku ya kichipuka”, wimbo huo unaonesha hisia za watu za kutarajia siku za kichipuka, na kutaka siku za kichipuka ziwe ndefu ili walime mashamba mazuri na kupata mavuno baadaye.

Kabila la waman (wengi wanaishi katika mikoa mitatu ya kaskazini mashariki pamoja na Beijing na mkoa wa Hebei): waman hupenda kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina mara mbili katika siku ya mkesha na siku ya tarehe 1 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo. Kabla ya sikukuu hiyo, waman hufanya mashindano ya kuruka kutoka kwenye farasi, na ngamia.

Kabila la watong (wengi wanaishi katika sehemu ya mkoa wa Guizhou, kusini magharibi ya China): watong hupenda kuvua samaki

asubuhi ya tarehe 1 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo na kuwaweka samaki hao hai kwenye meza ili kuonesha kuwa katika mwaka mpya familia itakuwa na baraka na chakula cha kutosha.

Kabila la wazhuan (wengi wanaishi katika mkoa unaojiendesha wa kabila la wazhuang la Guangxi, kusini magharibi ya China): wazhuang hupenda kupika chakula cha tarehe 1 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo usiku wa siku ya mkesha, kwa kuonesha kuwa mwaka unaofuata watakuwa na mavuno na baraka.

Kabila la waqiang (wengi wanaishi mkoani Sichuan, kusini magharibi ya China): wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina, kila familia za waqiang huweka sadaka za ng'ombe na kondoo kwa kutambika kwa mababu. Aidha, katika usiku wa mkesha wa sikukuu, watu wote wa kila familia wakae pamoja kwa kuzunguka chungu cha pombe, mwenye umri mkubwa zaidi akinywa pombe kwanza kwa mrija wa mita moja halafu watu wa familia hiyo wanafyonza pombe kwa zamu toka kushoto hadi kulia.

Kabila la washui (wengi wanaishi mkoani wa Guizhou, kusini magharibi ya China): wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi, watoto wa kabila la washui wanaweza kuomba peremende kwa wazazi wa kila familia, nani atakaye pata peremende nyingi atachukuliwa kuwa ni mtoto mwenye heri na baraka zaidi, na siku za usoni atakuwa ni mwenye akili na afya nzuri.

Kabila la wabai (wengi wanaishi mkoani Yunnan, kusini magharibi ya China): Asubuhi ya Tarehe 1 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo ya kichina, wabai wote wazee kwa watoto wa kila familia hunywa maji ya sukari yaliyotiwa mchele, hii inaonesha kuwa katika mwaka mpya wataishi maisha matamu.

Kabila la wakorea (wengi wanaishi katika mkoa wa Jilin, kaskazini mashariki ya China): Katika sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina, watu wa kabila la wakorea wa kila familia wanabandika karatasi zilizoandikwa maneno ya kutakia heri na baraka za mwaka huu kwenye milango ya nyumba, kupika vyakula vingi vya aina mbalimbali. Na asubuhi mapema ya tarehe 1 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo, watu huamka na kuvaa nguo maridadi ya sikukuu na kutoa heshima kwa wazee na wazazi na kuwatakia heri na baraka za mwaka mpya.

Kabila la wamongolia (wengi wanaishi katika mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani ya kaskazini magharibi ya China): Asubuhi ya tarehe 1 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo, vijana wa kiume na kike wanaovaa nguo maridadi za aina mbalimbali hupanda farasi kwenda nyumbani kwa wazazi wa kila familia kutoa heshima na kuwatakia heri na baraka za mwaka mpya. Aidha, kabila la wamongolia hufanya tamasha kubwa la kuimba nyimbo na kucheza ngoma, ambapo watu wote wanavaa vibandiko kwenye nyuso zao, ili kuonesha kuagana na mwaka uliopita na kukaribisha mwaka mpya.

Kabila la wahani (wengi wanaishi mkoani Yunnan, kusini magharibi ya China): vijana wa kiume na kike wa kabila la wahani hukusanyika pamoja wakati wa mwaka mpya wa jadi wa kichina, wakinywa pombe, kuimba nyimbo, kucheza dansi na kuwachagua wachumba.

Kabila la Wanaxi (mkoani Yunnan, kusini magharibi mwa China): Katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa Kichina, watoto wa kiume wanaotimiza miaka 13 wanafanyiwa “sherehe ya kuvaa suruali” na watoto wa kike wanafanyiwa “sherehe ya kuvaa sketi”, ikimaanisha kuwa watoto hao wameingia katika utu uzima.

Kabila la Wapumi (mikoani Yunnan na Sichuan, kusini magharibi mwa China):

Asubuhi katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa Kichina watu wa kabila la Wapumi wanapiga mizinga na mbiu kuusherehekea mwaka mpya.

Kabila la Wabuyi (mkoani Guizhou, kusini magharibi mwa China):

Katika siku za mwaka mpya wa Kichina vijana wa kabila hilo huvaa mavazi ya sikukuu kusalimiana au kwenda kufanya utalii, kuimba na kucheza ngoma vya kutosha, kisha wanarudi nyumbani.

Kabila la Waoroqen (mkoani Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China):

Asubuhi mapema katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa Kichina vijana wa kabila hilo huwamiminia wazee wa familia yao glasi nzima ya mvinyo wakionesha heshima, kisha vijana hao wanatakiana heri kwa kunywa mvinyo. Baada ya kifungua kinywa vijana hukusanyika pamoja kufanya mashindano ya mbio za farasi na kulenga shabaha kwa mishale.

Kabila la Wadaur (mkoani Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China):

Asubuhi mapema katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa Kichina vijana wa kabila la Wadaur huwa wanapaka masizi na kuwapakia wengine usoni wakiwemo wasichana. Inasemekana kuwa kufanya hivyo kuna maana ya kuwatakia furaha na mavuno mazuri ya kilimo.