Masimulizi kuhusu mkesha wa mwaka mpya
中国国际广播电台

      Usiku wa siku ya mwisho ya Desemba katika kalenda ya Kichina ni mkesha sikukuu ya mwaka mpya wa Kichina.

Katika usiku huo wa kuamkia sikukuu ya mwaka mpya, mila na desturi za Wachina ni nyingi. Moja ni kufagia nyumba. Kabla ya kufikia siku ya mwisho ya mwaka watu hufagia nyumba kwa maana ya kuondoa uchafu na kusherehekea mwaka mpya katika hali ya kila kitu kuwa safi.

Baada ya kusafisha, wanapamba nyumba kwa maandishi yenye maneno ya kuomba baraka na picha, na kutundika taa nyekundu.

Katika mkesha wa mwaka mpya, jamaa hula pamoja, hata fulani akiwa mbali kwa kazi lakini katika siku hiyo hurudi nyumbani kujumuika na jamaa zake na kula nao pamoja.

Chakula cha usiku wa kuamkia sikukuu ya mwaka mpya katika sehemu ya kusini na sehemu ya kaskazini ni tofauti. Watu wa sehemu ya kusini hupika vitoweo vingi zaidi na kumi na watu wa sehemu ya kaskazini wana mila ya kula Jiaozi kwa kuchovya kwenye siki iliyotiwa saumu.

Katika usiku huo watu wazima huwachukua watoto na kwenda nao kwa jamaa na kuwapelekea zawadi, na watoto katika usiku huo wanawasibiliza wazee wosia wao. Katika usiku huo watoto hupewa fedha ambazo zinaitwa “fedha za kuaga mwaka”. Si wazee si watoto, katika usiku huo hawalali, baada ya chakula, wanaongea huku wana wanakunywa chai na kula vyakula vya udohodoho na kuangalia michezo ya televisheni mpaka alfajiri.

Katika usiku huo watoto huwa na furaha tele, wanapitisha usiku huo wakiwa pamoja na wazee na kuwasha fataki. Mshairi mkubwa wa China ya kale aliwahi kueleza watoto walivyokuwa katika usiku huo “Watoto wavumilia usingizi na kuwa na furaha hadi alfajiri”.