Siku ya Mwisho ya Majira ya Baridi
中国国际广播电台

   “Siku ya Mwisho ya Majira ya Baridi” ni moja katika vipindi 24 vya majira katika kalenda ya Kichina. Mapema miaka elfu mbili na saba iliyopita watu wa China ya kale walikuwa na siku hiyo.

“Siku ya mwisho ya majira ya baridi” haimaanishi kwamba katika siku hiyo jotoridi ni chini kabisa, bali inamaanisha dunia imefika mahali fulani katika njia yake ya kulizunguka jua. Katika siku hiyo, mchana ni mfupi kabisa katika mwaka mzima, na baada ya siku hiyo muda wa mchana unakuwa mrefu siku hadi siku. Katika China ya kale wafalme walikuwa wanafanya sherehe kwa siku tano na kufanya tambiko katika hekalu la Tiantan mjini Beijing.

“Siku ya Mwisho ya Majira ya Baridi” watu pia wanaita “mwanzo wa siku tisa tisa”. Watu wanaanza kuhesabu siku tisa tisa kuanzia siku hiyo, jumla kuna “siku tisa tisa” tisa, yaani siku 81, na majira ya Spring huanza kabla ya “siku tisa tisa” ya sita.

Miongoni mwa wenyeji baadhi ya watu wana desturi ya kupaka rangi kwenye maua, jumla maua 81, kila baada ya siku moja kupita wanatia rangi kwenye ua moja mpaka maua yote 81 yapakwe rangi ambapo majira ya Spring yanakuwa yamefika na jitoridi linakuwa la uvuguvugu.