Siku Safi na Angavu
中国国际广播电台

      Siku Safi ya Angavu iko katika mwanzoni mwa majira ya Spring.

Siku Safi na Angavu ni moja katika vipindi vya majira 24 katika kalenda ya Kichina, siku hiyo iko mwanzoni mwa mwezi Aprili. Katika siku hiyo watu huenda kutembelea viungani au kwenda kusafisha makaburi kuwakumbuka marehemu.

Katika siku kabla na baada ya Siku Safi na Angavu, watu huwa wanakwenda kwenye makaburi kutoa heshima kwa wazee waliokufa. Kwenye makaburi wanaondoa majani, wanachoma karatasi zilizokatwa kama noti na kupiga magoti au kusimama kimya kuwakumbuka marehemu kwa dakika chache.

Kuwakumbuka marehemu katika siku hiyo kulianzia Enzi ya Han (206 K.K.--220 K,K.), na katika enzi za Ming na Qing (1368—1911) shughuli za kusafisha makaburi zilipamba moto, na baadhi ya watu licha ya kusafisha makaburi, wnapika vyakula kuweka mbele ya makaburi.

Kusafisha makaburi kumekuwa mila ya Wachina katika siku hiyo na kuendelea mpaka leo, ila tu licha ya kuwakumbuka marehemu pia wanakwenda kwenye makaburi ya mashujaa na kuweka mashada ya maua kuonesha heshima zao.

Kwa sababu kipindi cha Siku Safi na Angavu ni mwanzo wa majira ya Spring, watu hufanya utalii katika viunga vya miji kuburudika mazingira ya kuchipua kwa majani na kupunga upepo mzuri.

Katika China ya kale wanawake walikuwa na desturi ya kuchuma mboga msituni na kutengeneza Jiaozi na kuchomeka maua kichwani.

Katika kipindi cha Siku Safi na Angavu watu pia wana desturi ya kurusha tiara, kucheza mchezo wa kuvutana kwa kamba na kubembea.

Lakini kwa nini siku hiyo inaitwa Siku Safi na Angavu? Kwa sababu katika kipindi hicho majira ya Spring imeanza, mbingu ni safi na jua si kali, majani yameanza kuchipuka, na watu wameanza kupanda mbegu na miti.

Katika China ya kale watu walikuwa na desturi ya kupanda miti katika sehemu za makazi yao.