Desturi ya Kunywa Chai
中国国际广播电台

      Wachina wamekuwa na historia ya miaka elfu nne ya kunywa chai. Chai ni kitu ambacho hakiwezi kukosekana katika maisha ya kila siku ya Wachina. Wageni wanapofika nyumbani kwa mtu fulani, nao hukaribishwa kwa chai, wanaongea na mwenyeji na huku wanakunywa chai.

Katika Enzi ya Tang kunywa chai kulianza kuwa desturia ya Wachina. Inasemekana kwamba desturi hiyo inahusiana na dini ya Buddha. Mwaka 713 hadi 741, sufii wa dini ya Buddha waliosoma msahafu kwa muda mrefu walikuwa wanajisikia usingizi, basi sufii mzee aliwataka wanywe chai. Tokea hapo njia hiyo ya kuondoa usingizi ilienea kila mahali.

Mwaka 780 mtaalamu wa chai aliandika kitabu cha namna ya kulima, na kutengeneza majani na kunywa chai. Na katika Enzi ya Song mfalme alikuwa anawakaribisha wageni kwa chai.

Nchini China kunywa chai ni aina moja ya utamaduni. Tokea enzi na dahari hadi leo mikahawa ya chai hupatikana kila mahali nchini China, na katika sehemu ya kusini pia kuna vibanda vya chai. Watu wanakunywa chai huku wakiburudika na michezo ya sanaa.

Wachina wa sehemu tofauti pia wana desturi ya kunywa chai tofauti. Watu wa sehemu ya kaskazini wanapenda kunywa chai ya jasmini, watu wa kusini wanapenda kunywa chai ya kijani na baadhi ya watu wanapenda kunywa chai nyekundu.

Namna ya kunywa chai pia ni tofauti kutokana na sehemu tofauti. Watu wa sehemu ya mashariki ya China wanapenda kutumia bilauri kubwa na kutia majani ya chai ndani yake na kisha kumimina ndani ya glasi. Na watu wa sehemu ya kusini wanapenda kumimina maji ya moto ndani ya glasi na kutia majani ndani yake.

Adabu ya kunywa chai pia ni inatofautiana kutokana na sehemu tofauti. Mjini Beijing, mwenyeji akileta glasi ya chai, mgeni husimama kuipokea kwa kuonesha heshima na kusema “ahsante”. Katika sehemu ya kusini mwenyeji akileta glasi ya chai, mgeni hugongagonga meza mara tatu kwa kidole kuonesha shukrani.