Historia ya Opera ya Kibejing
中国国际广播电台

      Opera ya Kibeijing inasifiwa kama ni opera ya Mashariki. Opera ya Kibeijing imekuwa na historia ya miaka zaidi ya 200. Asili yake ni opera ya kisehemu katika zama za kale. Mwaka 1790 kikundi cha opera ya Hui kiliingia mjini Beijing na kuonesha michezo kwa ajili ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mfalme.

 

 

   Mwishoni mwa karne ya 19 baada ya kupokea mitindo ya aina mbalimbali za opera nyingine za kisehemu , Opera ya Kibeijing imekuwa kama ya sasa. Opera ya Kibeijing ni mkusanyiko wa sanaa nyingi, zikiwa ni pamoja na “kuimba, kuongea, kuiga, kupigana, na kucheza dansi”. Nafasi za waigizaji zinagawanyika: Sheng (kwa wanaume), Dan (kwa wanawake), Jing (kwa wanaume) na Chou (kwa wanaume na wanawake). Michoro ya usoni ni aina maalumu ya opera ya Kieijing. Kutokana na michoro tofauti watu, wanafahamu kama ni watu wabaya na wenye heshima. Kwa mfano, michoro ya rangi nyekundu inaonesha mtu mwaminifu, rangi ya zambarau inaonesha mtu mwenye ujasiri, rangi nyeusi inaonesha mtu mwenye unyoofu, rangi nyeupe inaonesha mwenye hila, rangi ya buluu inaonesha mtu mwenye ujasiri, rangi ya manjano inaonesha mwenye ukatili na rangi ya fedha inaonesha mashetani, miungu. Opera ya Kibeijing ilipamba moto katika karne ya 18. wachezaji mashuhuri wa Opera ya Kibeijing ni Bw. Mei Lanfang (1894-1961), Shang Xiaoyun (1900-1975), Cheng Yanqiu (1904-1958) na Xun Huisheng (1900-1968). Bw. Mei Lanfang anajulikana sana duniani, alianza kucheza opera ya Kibeijing tokea alipokuwa na umri wa miaka minane, na kuanza kucheza jukwaani alipokuwa na umri wa miaka 11. katika muda wake wa miaka zaidi ya hamsini jukwani alivumbua sanaa maalumu ya opera hiyo. Mwaka 1919 alitembelea Marekani akiwa pamoja na wenzake na kuonesha michezo yake, alipata mafanikio makubwa. Mwaka 1934 kutokana na mwaliko alikwenda Ulaya kuonesha michezo yake.

Baada ya China kuanza kufanya mageuzi kiuchumi opera ya Kibeijing imepata maendeleo mapya kwa kusaidiwa na serikali. hivi sasa michezo ya opera ya Kibeijing katika Jumba la Opera ya Kibejing la Chang An mjini Beijing, na maonesho ya kimataifa ya opera ya Kibeijing yanayofanyika kila mwaka yanavutia watazamaji wengi. Opera ya Kibeijing ni kama daraja la mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na nchi za nje.