Opera ya Kun
中国国际广播电台

      Opera ya Kun inaimbwa kwa lafudhi ya sehemu ya kusini ya China. Aina hiyo ya ilianzia mkoani Jiangsu katika sehemu ya mlima Kun, kwa hiyo inaitwa opera ya Kun .

Opera hiyo ilifika kileleni katika Enzi ya Ming na Qing. Katika kipindi hicho michezo iliyotungwa kwa ajili ya opera hiyo ilikuwa mingi, na walitokea wachezaji wengi hodari.

Lugha inayotumika katika opera hiyo ni nzuri sana, bila kuangalia opera yenyewe, hata ukisoma maandishi ya michezo utafurahia lugha yake nzuri.

Opera ya aina hiyo huoneshwa kwa kuimba na kucheza kwa kushirikiana na bendi.

Maendeleo ya opera ya Kun yaliathiri sana opera za aina nyingine kama za Chuan , Xiang , Yue , na Huangmei . Watu husema, opera ya Kun ni asili ya opera zote nchini China.