Opera ya Yu
中国国际广播电台

      Opera ya Yu imeenea sana katika mikoa ya Henan, Hebei, Shandong, Shanxi, Hubei, Ningxia, Qinghai na Xinjiang, ni moja kati ya opera muhimu nchini China.

Opera hiyo ilianza mwishoni mwa Enzi ya Ming na mwanzoni mwa Enzi ya Qing.

Bendi ya opera hiyo huwa na ala za muziki za erhu , sanxian , pipa , filimbi, sheng na tarumbeta.

Opera hiyo huchezwa kwa kuimba, inaeleza wazi hisia za mtu, na michezo inayooneshwa kwa opera hiyo huwa ni maisha ya kila siku ya raia, ikionesha hadithi tokea mwanzo mpaka mwisho.

Kabla ya mwaka 1927 opera hiyo ilikuwa haina wachezaji wanawake. Baadaye walitokea wachezaji hodari na maarufu sana kama Chang Xiangyu, Chen Suzhen, Ma Jinfeng, Yan Lipin, Cui Lantian ambao wanajulikana kote nchini China.

Kuna michezo ya jadi ya opera ya Yu zaidi ya 1000, na mingi inaeleza mambo ya historia. Baada ya Jamhuri ya Watu wa China kuasisiwa, michezo inayoeleza maisha ya zama za leo ilianza kutokea.

Hivi sasa ingawa opera hiyo inavutia sana watu wengi, lakini imekumbwa na matatizo, kwamba idadi ya watazamaji imepungua, vikundi vya opera hiyo vina matatizo ya kifedha, na wachezaji wanapungua.