Mtoto Yatima Zhao
中国国际广播电台

      Karne ya 8 hadi 5 K.K. kilikuwa ni kipindi cha Spring na Autumn, kulikuwa na madola mengi, na kati ya madola hayo kulikuwa na Dola la Jin. Katika dola hilo walikuwepo maofisa wawili wakubwa, mmoja ni wa ukatibu aliyekuwa mwaminifu kwa mfalme, aliitwa Zhao Dun, na mwingine ni ofisa wa jeshi aliyeitwa Tu Angu. Watu hao wawili walikuwa hawaelewani. Tu Angu alitaka kumwua Zhao Dun kwa hila.

Tu Angu alichemsha ubongo namna ya kumwua Zhao Dun kwa hila. Mfalme wa Dola la Jin kweli alidanganywa akiamini kuwa Zhao Dun ni msaliti wa taifa, aliamuru kumwua na watu wote wa familia yake isipokuwa mkamwana wake Zhuang Ji, kwa kuwa yeye ni binti wa mfalme lakini alifungiwa kwenye kasri.

Wakti huo Zhuang Ji alikuwa mja mzito na muda mfupi baadaye alizaa mtoto mmoja wa kiume, aliitwa “Mtoto Yatima Zhao”, mama yake alitumai kuwa mtoto huyo atalipiza kisasi kwa ajili ya familia ya Zhao. Ofisa Tu Angu alipata habari kuwa binti wa mfalme alizaa mtoto, alituma watu kulinda mlango wa kasri na kumwua mtoto huyo alipotimiza mwezi mmoja ili kufyeka mzizi utakaohatarisha usalama wake baadaye.

Zhao Dun alikuwa na rafiki mmoja mkubwa kwa jina la Cheng Ying, alikuwa ni daktari. Ili kumwokoa mtoto huyo yatima, alibeba sanduku lake la dawa alijidai kwenda kumtibu binti wa mfalme. Alitia mtoto ndani ya sanduku lake na kutaka kumtorosha nje ya kasri. Lakini alipofika kwenye mlango wa kasri aligunduliwa na jemadari Han Jue aliyelinda mlango. Han Jue pia alimhurumia sana mtoto huyo alimwachia huru, lakini yeye mwenyewe alijiua kwa kisu.

  Tu Angu alipofahamu kuwa mtoto ametoroshwa, akaamuru kwamba kama katika muda wa siku tatu mtoto huyo hajagunduliwa atawaua watoto wote nchini walio chini ya umri wa mwaka moja.

Cheng Ying alishauriana na rafiki mwingine wa Zhao Dun aliyeitwa Gong Sunchujiu, waliona kuwa njia moja tu ya kuweza kuwaokoa watoto wote wa dola la Jin, nayo ni kumwacha mtoto mmoja mwingine auawe badala ya mtoto yatima. Cheng Ying alikuwa na mtoto mmoja ambaye alilingana na mtoto yatima kwa umri. Basi Cheng Ying kwa uchungu alimpa Gong Sunchujiu mtoto wake na alikwenda kupiga ripoti kwa kusema kuwa Gong Sunchujiu alimficha mtoto yatima. Basi Gong Sunchujiu na mtoto wote waliuawa.

Miaka 15 baadaye, jemadari mwaminifu Wei Jiang alikuja kutoka mpakani, aliposikia kwamba watu wa familia Zhao Dun wote waliuawa na Cheng Ying alipiga ripoti alikasirika sana hata alimchapa viboko vikali Cheng Ying.

Cheng Ying alikuwa kimya alipochapwa viboko, akifikiri kuwa viboko vikali vinaonesha chuki zake kwa msaliti, na atasaidia mtoto yatima kulipa kisasi. Baada ya kubaini uaminifu wa Wei Jiang alimwambia yote jinsi alimtoa mtoto wake na Gong Sunchujiu alivyouawa kwa ajili ya kumwokoa mtoto yatima. Wei Jiang alisisimka na kumwahidi atamsaidia mtoto yatima kulipiza kisasi.

Baada ya kurudi nyumbani Cheng Ying alimwambia yote ya zamani kwa picha. Mtoto yatima alielewa kisa chake akadhamiria kulipiza kisasi.