Mapenzi ya Dhiki
中国国际广播电台

     Mke wa Zhong Shanwang aliyeitwa Liang Qi kwa kuogopa kupoteza mapenzi ya mumewe kwa kutokuwa na mtoto wa kiume, alibadilishana mtoto wake wa kike aliyezaliwa siku chache kwa mtoto wa kiume na kuchapa alama nyekundu kwenye bega la mtoto wake halisi wa kike. Mtoto aliyepata alimpatia jina la Xu Tian Bao.

Baada ya miaka 18 mhuni mmoja aliyeitwa Chang Ming siku moja alivamina na kumpora mwimbaji mwanamke Li Ying na alimwua baba yake, lakini baadaye Xu Tianbao alimwokoa mwimbaji huyo Li Ying. Kutokana na kuhofu kuwa mhuni Chang Ming atalipiza kisasi, alimficha nyumbani kwa mtu, siku nenda siku rudi walikuwa na mapenzi, na waliahidiana kufunga ndoa baadaye. Lakini mama wa Tian Bao alimdharau Li Ying aliyetoka ukoo maskini, alikwenda kwa mwimbaji huyo na kumpiga, ghafla aligundua alama nyekundu begani. Wakati huo mfalme alimchagua Tian Bao kuwa mume wa binti yake. Tian Bao alikuwa hana njia ila kukubali lakini moyoni aliendelea kumpenda Li Ying na kumpuuza binti wa mfalme. Binti wa mfalme alikasirika, alitaka kumwua Li Ying, Tian Bao alimpiga katika ugomvi.

Binti wa mfalme alimshitaki Tian Bao kwa baba yake, mwanzoni mfalme alipouliza alifikiri ni ugomvi wa kawaida tu kati ya mume na mke waliooana, alipuuza. Mhuni Chang Ming alikuwa siku zote alikuwa na chuki Tian Bao, alimshawishi mfalme amwue kutokana na ugomvi wao, mfalme alitaka kumwua Li Ying. Mama wa Tian Bao alimhurumia sana binti yake halisi, alimweleza ukweli wa mambo kwamba Li Ying ni binti Xu Dong, mfalme alighadhibika vibaya, alitaka kuinua familia ya Xu Dong na kumwua Tian Bao, aliyesimamia uuaji huo alikuwa Chang Ming.

Katika mahali pa kuulia, Li Ying na Tian Bao waliahidiana kuwa Tian Bao akiuawa Li Ying pia atajinyonga nyumbani. Lakini dakika kabla ya uuaji kutekelezwa, binti wa mfalme alikuja haraka na amri ya mfalme, kwamba Tian Bao amesamehewa adhabu ya kifo na aendelee kuwa mume wa binti yake. Lakini ngoma ilipigwa kuashiria uuaji ufanywe, Li Ying aliposikia vishindo vya ngoma alijinyonga.

Tian Bao alimchukua Li Ying mikononi akipiga hatua pole pole huku akitokwa na machozi.