Fadhili ya Punda na Wema wa Kisura
中国国际广播电台

     Mganga aliyestaafu wa mfalme Zhou Hongde alikuwa na johari moja ambayo inaweza kugundua na kutibu magunjwa. Siku moja mafuriko yalipotokea mganga huyo alimwokoa kijana mmoja aitwaye Liao Zhongping na kumchukua kuwa ni mwana wake wa kulea. Wakati huo alipashwa habari kuwa mama mfalme anaumwa na dawa zote hazikumsaidia. Basi mganga mstaafu Zhou Hongde aliwaagiza mtoto wake halisi Yao Nian na mtoto wake wa kulea Liao Zhongping waende pamoja kwa mama mfalme wakiwa na johari yake. Ili kupata johari, njiani Liao Zhongping alimsukuma gengeni Yao Nian, na alienda kumganga mama mfalme kwa johari aliyoinyakua. Mama mfalme akapona, Liao Zhongping alirudi na sifa tele na mavazi ya fahari, aliteuliwa kuwa mtemi mkubwa, na alitangaza kuwa Yao Nian alianguka na kufa gengeni walipokuwa njiani, na alichoma moto nyumba ya baba yake mlezi Zhou Hongde na kumnyang'anya mtoto wa kike wa kulea Wan Qing kuwa mke wake, na huyo Wan Qing alijitupa mtoni kujiua.

Mganga mstaafu Zhou Hongde alikuwa mgonjwa kutokana na msiba na hasira, na alidaiwa madeni mengi kutokana na ugonjwa wake. Mke wa Zhou Zhaonian, Shu Xian, alilazimika kuolewa na jemadari mmoja aliyeitwa Xiong Yemeng kuwa mke wa pili ili aweze kuwaokoa wanafamilia wazee na watoto. Katika siku ya ndoa, jemadari Xiong Yemeng alipata amri ya kwenda kupambana na maadui mpakani, akamwagiza Shu Xian amlee mtoto wake mdogo Xiong He-en.

Baada ya miaka minane, mtoto wake halisi Zhou Xiaoping na mtoto wa jemadari Xiong He-en walikuwa watu wazima na wote walikuwa maofisa. Na Zhou Zhaonian aliyesukumwa gengeni aliokolewa na amekuwa jemadari. Katika ushirikiano wa mapambano majemadari hao wawili waliweka urafiki mkubwa. Katika karamu ya kusherehekea ushindi Zhou Zhaonian alikutana na mkewe Shu Xian. Majemadari wawili hao waligombania mke. Baada ya kuelezana mambo yaliyopita, ukweli ukawa umedhihirika. Mwishowe Liao Zhongpia aliadhibiwa kisheria, na jemadari Xiong Yemeng alimwoa msichana Wan Qing aliyeokolewa kutoka mtoni. Jamaa wa familia ya Zhou wakajiunga pamoja.