Bunge la umma la China

中国国际广播电台Utaratibu wa Bunge la umma la China ni utaratibu wa kisiasa wa kimsingi wa China. Bunge la umma la China ni chombo chenye madaraka ya juu kabisa la taifa, ambalo linaundwa na wajumbe waliochaguliwa kutoka mikoa, mikoa inayojiendesha, miji inayotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu, mikoa ya utawala maalum na jeshi. Chombo hicho kinaendesha madaraka ya taifa ya utungaji wa sheria na kuamua masuala makubwa ya maisha ya siasa ya taifa.

Madaraka makuu ya Bunge la umma la China ni: Kurekebisha katiba, kusimamia utekelezaji wa katiba, kutunga na kurekebisha sheria za makosa ya jinai, mambo ya raia, idara za taifa na sheria nyingine za kimsingi; kuthibitisha na kuidhinisha mipango ya maendeleo ya uchumi na jamii na ripoti kuhusu hali ya utekelezaji wa mipango, pamoja na bajeti ya taifa na ripoti kuhusu hali ya utekelezaji wa bajeti ya taifa; kuidhinisha kuanzishwa na kuwekwa kwa mikoa, mikoa inayojiendesha na miji inayotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu, na kuamua uanzishaji wa mkoa wa utawala maalum na mfumo wake; kuamua masuala kuhusu vita na amani; kuchagua na kuamua viongozi wa chombo chenye madaraka ya juu kabisa cha taifa, yaani kuchagua wajumbe wa Halmashauri ya kudumu ya Bunge la umma la China na wajumbe wa bunge hilo, kuwachagua rais, makamu wa rais wa nchi, kuamua waziri mkuu wa serikali na viongozi wengine, kuchagua mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi na viongozi wengine wa kamati hiyo, kumchagua mkuu wa mahakama kuu ya umma na kumchagua mkuu wa Idara kuu ya uendeshaji wa mashitaka. Bunge la umma la China lina madaraka ya kuwaondoa madarakani viongozi wote hao waliotajwa.

Muda wa Bunge la umma la China la kila awamu ni miaka mitano, bunge hilo linafanya mkutano wa wajumbe wote kila mwaka. Wakati mkutano huo unapofungwa, Halamshauri yake ya kudumu inaendesha madaraja ya juu kabisa ya taifa. Halamshauri ya kudumu ya Bunge la umma la China linaundwa na spika, manaibu maspika, katibu mkuu na wajumbe.

Utungaji sheria wa China ni pamoja na utungaji sheria wa Bunge la umma la China na halmashauri yake ya kudumu, utungaji sheria wa Baraza la serikali na wizara zake, utungaji sheria wa kawaida wa mikoa mbalimbali, utungaji sheria wa mikoa inayojiendesha ya makabila madogomadogo, utungaji sheria wa sehemu maalum za kiuchumi na mikoa ya utawala maalum.