中国国际广播电台
Baraza la mashauriano ya kisiasa
la umma la China ni jumuia
ya wazalendo wanaopenda nchi
ambalo ni baraza muhimu la
kufanya ushirikiano wa vyama
vingi na mashauriano ya kisiasa
chini ya uongozi wa Chama
cha kikomunisti cha China,
ambapo wajumbe wa jumuia hiyo
wanaweza kuenzi demokrasia
ya ujamaa katika maisha ya
siasa ya China. Mshikamano
na demokrasia ni mada kubwa
mbili za baraza hilo.
Halmashauri ya nchi zima ya
Baraza la mashauriano ya kisiasa
la umma la China inaundwa
na wajumbe wa Chama cha kikomunisti
cha China, vyama mbalimbali
vya kidemokrasia, watu wasio
na vyama, makundi ya umma,
wajumbe wa makabila madogomadogo
na wajumbe wa sekta mbalimbali,
ndugu wa mikoa ya utawala
maalum ya Hong Kong na Makau,
ndugu wa Taiwan na wachina
walioishi nchi za nje pamoja
na watu walioalikwa maalum.
Muda wa kila awamu ya halmashauri
hiyo ni miaka mitano.
Jukumu kubwa la halmashauri
hiyo na ya ngazi mbalimbali
ni kufanya mashauriano ya
kisiasa, usimamizi wa demokrasia,
kutoa maoni na mapendekezo
kuhusu sera za nchi na maazimio
ya serikali.
Mashariano ya kisiasa
Kabla ya serikali kuu na serikali
za mikoa kutoa sera na maazimio
kuhusu masuala makubwa ya
siasa, uchumi, utamaduni na
jamii, Halmashauri ya nchi
nzima ya Baraza la mashauriano
ya kisiasa na halmashauri
ya mikoa zinaweza kuitisha
mikutano inayohudhuriwa na
wakuu wa vyama mbalimbali
na makundi mbalimbali pamoja
na wajumbe wa makabila na
sekta malimbali ili kufanya
mashauriano na kutoa maoni
na mapendekezo yao.
Usimamizi wa kidemokrasia:
Kutoa maoni na mapendekezo
au ukosoaji kwa kufanya usimamizi
kuhusu utekelezaji wa katiba
ya nchi, sheria na kanuni,
sera na hatua kubwa, kazi
za ofisi za serikali na watumishi
wake.
Kushiriki mambo ya siasa
Kufanya uchunguzi na utafiti
na kufanya majadiliano kwa
kutoa maoni ya wananchi kuhusu
masuala muhimu ya siasa, uchumi,
utamaduni na maisha ya jamii
pamoja na masuala yanayofuatiliwa
na umati wa watu. Kutoa ripoti
na miswada ya mapendekezo
au kupitia njia nyingi kwa
kutoa maoni na mapendekezo
kwa chama cha kikomunisti
cha China na idara za serikali
ya China.
Mwezi Septemba mwaka 1949,
Mkutano wa kwanza wa wajumbe
wote wa Baraza la mashauriano
ya kiasiasa la umma la China
uliendesha madaraka badala
ya Bunge la umma la China
na kuwakilisha nia ya wananchi
wa taifa zima, ukitangaza
kuanzishwa kwa Jamhuri ya
Watu wa China, hii ni kazi
muhimu ya historia iliyofanywa
na baraza hilo. Baada ya kufanyika
kwa mkutano wa kwanza wa Bunge
la umma la China mwaka 1954,
Baraza la mashauriano ya kisiasa
haliendeshi tena madaraka
ya Bunge la umma la China,
lakini limeendelea kuwepo
likiwa jumuiya ya wazalendo
wanaoipenda nchi, ambalo limefanya
kazi nyingi na kutoa mchango
mkubwa katika maisha ya kisiasa
ya taifa na maisha ya jamii
pamoja na shughuli za urafiki
kwa nchi za nje. Ilipofika
mwezi Machi mwaka 2004, baraza
hilo limeanzisha mawasiliano
na idara 170 za nchi 101 na
jumuia 8 za kimataifa au kikanda,
na kuanzisha mawasiliano ya
kirafiki.
|