中国国际广播电台
Mahakama kuu ya umma ni idara
ya taifa ya kushughulikia
kesi. Serikali inaweka mahakama
kuu ya umma, mikoa, mikoa
inayojiendesha na miji inayotawaliwa
moja kwa moja na serikali
kuu inaweka mahakama kuu ya
ngazi ya juu, mahakama ya
umma ya ngazi ya kati na mahakama
ya umma ya shina. Mahakama
kuu ya umma ni chombo cha
taifa cha hukumu cha ngazi
ya juu kabisa, ambayo inaendesha
madaraka ya uhukumu bila kuingiliwa,
vilevile ni mamlaka ya juu
kabisa ya usimamizi wa kazi
ya mahakama ya umma ya ngazi
mbalimbali. Mahakama kuu ya
umma inawajibika kwa Bunge
la umma la China na kutoa
ripoti kuhusu kazi yake kwa
bunge la umma, mkuu na naibu
mkuu wa Mahakama kuu ya umma
pamoja na wajumbe wa Kamati
ya utoaji hukuma wa Mahakama
kuu ya umma wote wanateuliwa
na kuamuliwa na Bunge la umma
la umma la China.
Jukumu la Mahakama kuu ya
umma ni kushughulikia kazi
ya utoaji hukumu kuhusu kesi
zilizotolewa rufaa juu ya
hukumu zilizotolewa na mahakama
za ngazi ya Chini au Idara
kuu ya uendeshaji wa mashitaka
ya umma kwa kufuata utaratibu
wa usimamizi wa hukumu; kuthibitisha
hukumu za vifo; kama kugundua
makosa katika hukumu zilizotolewa
na mahakama ya umma ya ngazi
mbalimbali, mahakama kuu ya
umma ina madaraka ya kuhukumu
au kuagiza mahakama ya ngazi
ya chini kuhukumu tena; kuthibitisha
uhalifu; na kutoa ufafanuzi
kuhusu namna ya kutumia sheria
halisi katika mchakato wa
hukumu na kadhalika.
Mkuu wa Mahakama kuu ya umma
wa sasa ni Bwana Xiao Yang.
。
|