中国国际广播电台
Idara ya uendeshaji wa mashitaka
ya umma ni mamlaka ya taifa
ya usimamizi wa sheria. Idara
hiyo inakamilisha jukumu lake
kwa kuendesha madaraka yake
ya uendeshaji wa mashitaka.
Idara hiyo inaendesha madaraka
yake katika kesi ya kuhaini
nchi, kufarakanisha taifa
na kesi nyingine kubwa; kufanya
ukaguzi na uthibitishaji kuhusu
kesi zilizoshughulikiwa na
idara za usalama wa umma,
kuamua kuwakamata watuhumiwa,
kuwashitaki au kutowashitaki;
kufanya usimamizi kuhusu shughuli
za idara za usalama wa umma,
mahakama ya umma, magereza
na idara husika za utekelezaji
wa sheria.
Idara kuu ya uendeshaji wa
mashitaka inaendesha madaraka
yake bila kuingiliwa kwa mujibu
wa sheria, kazi yake hairuhusiwi
kuingiliwa na idara za utawala,
makundi ya jamii au watu binafsi;
na inatekeleza sheria kwa
raia wote kwa usawa. Serikali
kuu inagawanyika katika Idara
kuu ya uendeshaji wa mashitaka
ya umma, idara za uendeshaji
wa mashitaka za mitaa za ngazi
mbalimbali na idara ya kijeshi
ya uendeshaji wa mashitaka.
Idara za uendeshaji wa mashitaka
za umma za China zinagawanyika
katika ngazi nne, yaani idara
za shina, idara ya ngazi ya
kati, idara ya ngazi ya juu
na idara kuu ya uendeshaji
mashitaka. Idara kuu ya uendeshaji
wa mashitaka ni idara ya juu
kabisa ya taifa yenye madaraka
ya kuendesha mashitaka, ikiwakilisha
taifa kuendesha madaraka ya
uendeshaji wa mashitaka kwa
kujiamulia, inawajibika moja
kwa moja kwa Halmashauri ya
kudumu ya Bunge la umma la
China. Jukumu lake kuu ni
kuongeza idara za uendeshaji
mashitaka za ngazi mbalimbali
za mitaa na idara maalum za
uendeshaji wa mashitaka kutekeleza
wajibu wake wa usimamizi wa
kisheria, na kuhakikisha kuwa
sheria za pamoja za taifa
na utekelezaji wake sahihi.
Mkuu wa sasa wa Idara kuu
ya uendeshaji wa mashitaka
ya umma ni Bwana Jia Chunwang.
|