Xi Jinping

Katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Mwenyekiti wa Kamati ya kijeshi ya Kamati kuu ya chama, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Naibu mwenyekiti wa Kamati kuu ya kijeshi ya Jamhuri ya Watu wa China, na Mkuu wa Chuo cha chama cha Kamati kuu ya chama.
Alizaliwa mwezi Juni mwaka 1953 huko Fuping mkoani Shaanxi, China. Alihitimu katika chuo cha utamaduni na jamii katika Chuo kikuu cha Qinghua, alipata digri ya uzamili na digri ya tatu ya sheria.
Aliwahi kuwa ofisa mwandamizi katika mikoa ya Hebei, Fujian, Zhejiang, na Shanghai kuanzia mwaka 1982 hadi mwaka 2007. Alikuwa Mjumbe wa Kamati kuu za 15 na 16 za Chama cha Kikomunisti cha China, Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya 17 ya chama. Alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China kwenye mkutano wa kwanza wa Bunge la umma la 11. Alichaguliwa kuwa Naibu mwenyekiti wa Kamati ya kijeshi ya Kamati kuu ya 17 ya Chama cha kikomunisti cha China, na kuchaguliwa kuwa Naibu mwenyekiti wa Kamati kuu ya kijeshi ya Jamhuri ya watu wa China kwenye Mkutano wa Bunge la umma la 11. Na kwenye Mkutano wa kwanza wa wajumbe wote wa Kamati kuu ya 18 ya chama, amechaguliwa kuwa Katibu mkuu wa Kamati kuu ya chama, na Mwenyekiti wa Kamati ya kijeshi ya Kamati kuu ya chama.