Li Keqiang

Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Naibu waziri mkuu, na Naibu katibu wa Kamati ya Chama.
Alizaliwa mwezi Julai mwaka 1955 huko Dingyuan mkoani Anhui,China. Alihitimu katika kitivo cha sheria na kitivo cha uchumi katika Chuo kikuu cha Beijing, alipata digri ya uzamili, digri ya kwanza ya sheria, na digri ya tatu ya uchumi.
Kuanzia mwaka 1982 hadi 1998 alikuwa Mjumbe wa kudumu wa Kamati kuu ya Umoja wa Vijana, Katibu na Katibu wa kwanza wa Ofisi ya Ukatibu ya Kamati kuu ya Umoja wa Vijana, Mkuu wa Chuo cha elimu ya siasa ya vijana cha China. Kuanzia mwaka 1998 hadi 2007 alikuwa ofisa mwandamizi wa mikoa ya Henan na Liaoning. Kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2012 amechaguliwa kuwa Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China, na Naibu waziri mkuu, na pia kushika nyadhifa mbalimbali.