Zhang Dejiang

Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Naibu waziri mkuu, Mjumbe wa Kamati ya chama, na Katibu wa Kamati ya chama ya Mji wa Chongqing.
Alizaliwa mwezi Novemba mwaka 1946 huko Taian, mkoani Liaoning, China. Alihitimu katika kitivo cha uchumi cha Chuo kikuu cha Kim Il Son cha Korea ya kaskazini.
Kuanzia mwaka 1970 hadi 2007 alikuwa ofisa mwandamizi katika mikoa ya Jinlin, Zhejiang na Guangdong. Mwaka 2002 hadi 2012 alikuwa Mjumbe wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya chama, Katibu wa Kamati ya Mji wa Chongqing.