Yu Zhengsheng

Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, na Katibu wa Kamati ya Chama ya Mji wa Shanghai.
Alizaliwa mwezi Aprili mwaka 1945 huko Shaoxing mkoani Zhejiang,China. Alihitimu katika Chuo kikuu cha Uhandisi wa kijeshi cha Harbin, na alikuwa mhandisi.
Kuanzia mwaka 1984 hadi 2008 alikuwa ofisa mwandamizi katika mikoa ya Shandong, Hubei na Shanghai, na alikuwa Waziri wa ujenzi. Kuanzia mwaka 2007 alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya chama.