Wang Qishan

Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Katibu wa Kamati kuu ya ukaguzi wa nidhamu, Naibu waziri mkuu, na Mjumbe wa Kamati ya Chama.
Alizaliwa mwezi Julai mwaka 1948 huko Tianzhen mkoani Shanxi, China. Alihitimu katika kitivo cha historia cha Chuo kikuu cha Kaskazini magharibi, alikuwa mtaalamu wa uchumi.
Kuanzia mwaka 1988 alikuwa mkuu katika benki mbalimbali, ofisa mwandamizi wa mikoa ya Guangdong, Hainan na Beijing. Kuanzia mwaka 2007 alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya chama, na naibu waziri mkuu.