Zhang Gaoli

Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, na Katibu wa Kamati ya Chama ya Mji wa Tianjin.
Alizaliwa mwezi Novemba mwaka 1946 huko Jinjiang mkoani Fujian, China. Alihitimu katika kitivo cha uchumi cha Chuo kikuu cha Xiamen.
Kuanzia mwaka 1984 hadi 2012 alikuwa ofisa mwandamizi wa mikoa ya Guangdong, Shandong na Tianjin. Kuanzia Mwaka 2007 alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya chama.