Vyama vya kidemokrasia vya China

中国国际广播电台


Nchini China mbali na Chama cha kikomunnisti cha China, pia kuna vyama vinane vya kisiasa yaani vyama vya kidemokrasia kama vile Kamati ya mapinduzi ya Chama cha Guomintang cha China, Umoja wa demokrasia wa China, Shirikisho la kujenga nchi ya kidemokrasia la China, Shirikisho la kuhimiza demokrasia la China, Chama cha demokrasia cha wakulima na wafanyakazi cha China, Chama cha Zhigong cha China, Shirikisho la elimu la Jiusan na Umoja wa kujiendesha kidemokrasia wa Taiwan. Vyama hivyo vingi vilianzishwa na kuendelea wakati wa mapambano dhidi ya uvamizi wa Japan na katika vita vya ukombozi wa nchi nzima. Vyama vya kidemokrasia vinaunga mkono uongozi wa Chama cha kikomunisti cha China, hili ni chaguo lao cha kihistoria katika ushirikiano wa muda mrefu na juhudi za pamoja. Vyama mbalimbali vya kidemokrasia vinafaidika na uhuru wa kisiasa, uhuru wa kujitawala kijumuia na usawa wa hadhi ya kisheria katika eneo lililowekwa kwenye katiba ya nchi. Chama cha kikomunisti cha China na vyama mbalimbali vya kidemokrasia vinafuata sera ya kimsingi ya ushirikiano ya “kuwepo kwa pamoja kwa muda mrefu, kusimamiana, kutendeana kwa moyo safi na udhati, na kushirikiana kwenye dhiki na faraja”.
Vyama mbalimbali vya kidemokrasia si vyama visivyo vya tawala, wala vyama vya upinzani, isipokuwa ni vyama vinavyoshiriki mambo ya kisiasa na utoaji wa sera. Hivi sasa wanachama wengi wa vyama mbalimbali vya kidemokrasia wanashika nyadhifa mbalimbali katika Bunge la umma la China na Baraza la mashauriano ya kisiasa kwenye ngazi mbalimbali, vyombo vya serikali na idara za uchumi, utamaduni, elimu, sayansi na teknolojia, kwa mfano wenyekiti wa kamati kuu ya vyama vinane vya kidemokrasia hivi sasa wanashika nyadhifa za manaibu spika wa Bunge la umma la China au manaibu wenyeviti wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China. Wakati huo huo, matawi ya vyama mbalimbali vya kidemokrasia pia yanaendelea vizuri katika mikoa na miji mbalimbali nchini China.

Kamati ya Mapinduzi ya Chama cha Guomintang cha China
Kamati ya Mapinduzi ya Chama cha Guomintang cha China kwa ufupi inaitwa Minge, ambacho kilianzishwa tarehe 1 Januari, mwaka 1948, kilianzishwa na kundi la kidemokrasia la Chama cha Guomintang cha China na wazalendo wengine, chama hicho kina umaalum wa shirikisho la kisiasa, ambacho ni chama kinachofanya juhudi katika kujenga ujamaa na kutimiza muungano wa taifa. Chama hicho kina wanachama karibu elfu 65. Mwenyekiti wa kamati kuu ya chama hicho ni Bibi He Luli.

Umoja wa demokrasia wa China
Umoja wa demokrasia wa China kwa ufupi unaitwa Minmeng, ambao ulianzishwa mwezi Machi, mwaka 1941, wakati huo umoja huo uliitwa “Shirikisho la vikundi vya kisiasa vya kidemokrasia la China”, mwaka 1944 uliundwa upya na kubadilisha jina kuwa Umoja wa demokrasia wa China. Umoja huo ni umoja wa kisiasa wa wasomi wanaoshughulikia mambo ya utamaduni na elimu na wazalendo wanaounga mkono ujamaa, na ni chama chenye malengo ya kijamaa. Idadi ya wanachama wake ni laki 1.56. Mwenyekiti wake ni Bwana Ding Shisun.

Shirikisho la kujenga nchi ya kidemokrasia la China
Kwa ufupi shirikisho hilo linaitwa Minjian, ambalo lilianzishwa mwezi Desemba mwaka 1945, wanachama wake wengi ni wanakampuni na wafanyabiashara wazalendo na wasomi wanaowasiliana nao. Wanachama wake wamefikia elfu 85. Mwenyekiti wake wa hivi sasa ni Bwana Cheng Siwei.

Shirikisho la uhimizaji wa demokrasia la China
Shirikisho hilo linaitwa Minjin kwa ufupi, ambalo lilianzishwa mwezi Desemba mwaka 1945, wanachama wake wengi ni wasomi wa kiwango cha juu na wastani wanaoshughulikia mambo ya elimu, utamaduni, uchapishaji vitabu na sayansi. Shirikisho hilo lina wanachama elfu 81. Mwenyekiti wake wa hivi sasa ni Bwana Xu Jialu.

Chama cha demokrasia cha wakulima na wafanyakazi cha China
Chama hicho kinaitwa chama cha Nonggong, ambacho kilianzishwa mwezi Agosti mwaka 1930. Chama hicho ni shirikisho la kisiasa la wasomi wa kiwango cha juu na wastani wanaoshughulikia mambo ya afya, sayansi na teknolojia na utamaduni na elimu pamoja na wazalengo wanaounga mkono ujamaa. Idadi ya wanachama wake ni zaidi ya elfu 80. Mwenyekiti wake wa hivi sasa ni Bwana Jiang Zhenghua.

Chama cha Zhigong cha China
Chama hicho kilianzishwa mwezi Oktoba mwaka 1925, ambacho kiliundwa na wachina waliowahi kuishi ng’ambo na jamaa zao. Idadi ya wanachama wake ni zaidi ya elfu 20. Mwenyekiti wake wa hivi sasa ni Bwana Luo Haocai.

Shirikisho la elimu la Jiusan
Chama hicho kilianzishwa mwezi Machi mwaka 1946, wanachama wake ni zaidi ya elfu 80 ambao ni wasomi wa kiwango cha juu na wastani wanaoshughulikia mambo ya sayansi na teknolojia, utamaduni na elimu pamoja na afya. Mwenyekiti wake wa hivi sasa ni Bwana Han Qide.

Umoja wa kujiendesha kidemokrasia wa Taiwan
Umoja huo unaitwa Taimeng kwa ufupi, ambao ulianzishwa mwezi Novemba mwaka 1947. Umoja huo ni shirikisho la kisiasa linaloundwa na wazalendo wanaounga mkono ujamaa wa mkoa wa Taiwan wanaoishi China bara. Mwenyekiti wake wa sasa ni Bwana Zhang Kehui.


Vikundi vya Jamii

Shirikisho kuu la wafanyakazi wa China
Shirikisho kuu la wafanyakazi wa China linaitwa Qiuanzong kwa ufupi, ambalo ni chombo cha uongozi cha mashirikisho ya wafanyakazi ya sehemu mbalimbali nchini China, ambalo lilianzishwa tarehe 1 Mei, mwaka 1925.

Jukumu la shirikisho hilo la jamii ni kulinda haki na maslahi halali ya wafanyakazi na haki zao za kidemokrasia; kuwahamasisha na kuwashirikisha wafanyakazi kushiriki katika ujenzi na mageuzi, kukamilisha majukumu ya maendeleo ya uchumi na jamii; kushiriki kwenye usimamizi wa kidemokrasia ya mashirika, na kuwaelimisha wafanyakazi wainue kiwango cha maadili na elimu ya sayansi, tekenolojia na utamaduni.

Shirikisho kuu la wafanyakazi wa taifa la China limeanzisha mawasiliano na uhusiano wa kirafiki na mashirikisho ya wafanyakazi ya kitaifa ya nchi na sehemu zaidi ya 130 duniani. Ilipofika mwishoni mwa mwaka 2002, idadi ya jumla ya wanachama wa shirikisho hilo imefikia milioni 134.
Mwenyekiti wa hivi sasa wa shirikisho hilo ni Bwana Wang Zhaoguo.

Shirikisho kuu la vijana la taifa la China
Shirikisho hilo lilianzishwa tarehe 4 Mei mwaka 1949 ambalo ni shirikisho la vijana wa makabila mbalimbali wa China.
Jukumu kuu la shirikisho hilo ni kuwakilisha na kulinda haki na maslahi ya vijana wa makabila mbalimbali na sekta mbaimbali za China; kuwaelekeza vijana wafanye juhudi na kushiriki kwenye maisha ya jamii, kufanya juhudi za kuwahudumia vijana kwa ajili ya ukuaji wao mzuri na kuwa watu wenye ujuzi kwa kulitumikia taifa; kuimarisha mawasilliano na mshikamano na vijana wa Taiwan, Hong Kong na Makau pamoja vijana wanaoishi ng’ambo; na kuendeleza mawasiliano na urafiki ma vijana wa nchi mbalimbali duniani.
Kamati ya nchi nzima ya shirikisho kuu la vijana ni chombo chenye madaraka ya juu kabisa, muda wake wa kila awamu ni miaka mitano. Kamati hiyo ina mwenyekiti mmoja na manaibu wenyeviti kadhaa. Wakati wa kufungwa kwa kamati hiyo, halmashauri ya kudumu ya kamati hiyo inaendesha shughuli zake za kila siku.
Shirikisho hilo linatekeleza utaratibu wa wanachama wa makundi, hivi sasa kuna wanachama wa makundi 48, wajumbe 1352, mwenyekiti wake wa hivi sasa ni Bwana Sun Jinlong.

Shirikisho kuu la kina mama wa taifa zima la China
Shirikisho hilo lilianzishwa mwezi Machi mwaka 1949, jina lake la mwanzoni ni Shirikisho kuu la kina mama la kidemokasia la taifa la China, mwaka 1957 jina lake lilibadilishwa kuwa Shirikisho kuu la kina mama la Jamhuri ya Watu wa China, mwaka 1978 jina lake lilibadilishwa kuwa Shirikisho kuu la kina mama la taifa zima la China. Jukumu lake la kimsingi ni: Kuleta mshikamano, kuhamasisha kina mama wengi washiriki katika ujenzi wa uchumi na maendeleo ya jamii, kuwakilisha na kulinda haki na maslahi ya kina mama, na kusukuma mbele usawa kati ya wanaume na wanawake.
Mwenyekiti wa sasa wa shirikisho kuu hilo ni Bibi Gu Xiulian.

Shirikisho kuu la viwanda na biashara la taifa la China
Shirikisho hilo lilianzishwa mwaka 1953, ambalo ni kundi la umma na shirikisho la biashara la kiraia lililoundwa na watu wa sekta za viwanda na biashara wa China.
Jukumu kuu la shirikisho hilo ni kushiriki kwenye mashauriano ya kisiasa, kutoa maoni na mapendekezo na kufanya usimamizi kuhusu sera na hatua kubwa za nchi na masuala makubwa kuhusu siasa, uchumi na maisha ya jamii; kuwaelekeza wanachama wake wafanye juhudi za kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi, kusukuma mbele kazi ya kukamilisha siku hadi siku mfumo wa uchumi wa soko huria wa ujamaa, kusukuma mbele maendeleo ya jamii kwenye sekta zote; kuwakilisha haki na maslahi halali ya wanachama wake, kueleza maoni, matakwa na mapendekezo ya wanachama wake; kutoa huduma mbalimbali kwa wanachama wake; kuanzisha mafunzo ya kazi maalum, kuwasaidia wanachama wake kuboresha usimamizi na uendeshaji wa shughuli, kukamilisha usimamizi wa kazi ya uhasibu, na kuinua teknolojia za uzalishaji na sifa za bidhaa; kuongeza mawasiliano na urafiki na mashirika ya viwanda na biashara na mikoa ya utawala maalum ya Hong Kong na Makau pamoja na sehemu ya Taiwan na ya nchi mbalimbali duniani, na kuhimiza ushirikiano katika sekta za uchumi, teknolojia na biashara.
Mwenyekiti wa sasa wa shirikisho hilo ni Bwana Huang Mengfu.