Picha ya "Kurudi Nyumbani kwa Kupanda Punda"
Radio China Kimataifa

Picha hiyo ilichorwa na Tang Bohu (1470-1523) wa Enzi ya Tang. Alikuwa mwenyeji wa mji wa Suzhou mkoani Jiangsu. Alikuwa hodari wa kuandika mashairi na kuchora picha. Alipokuwa mzee alianza kuamini dini ya Buddha.

Katika picha hiyo ilichorwa njia nyembamba vichakani, nyumba hapa na pale, mito iliyotiririka mlimani wenye miti mingi, na mtu mmoja aliyepanda punda akielekea nyumbani.