Kusimulia Hadithi kwa Kupiga Ngoma
Radio China Kimataifa

Sanamu hiyo ina kimo cha sentimita 55, ilitengenezwa katika Enzi ya Han Mashariki, na ilifukuliwa mkoani Sichuan, na sasa inahifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Taifa.

Sanamu nyingi za kale zilifukuliwa mkoani Sichuan na iliyo maarufu sana ni sanamu hiyo. Sanamu hiyo inaonesha mtu mwenye kichwa kikubwa kilichovaa kilemba na uso wenye makunyanzi tele. Ngoma ndogo kwenye mkono wa kushoto na mkono wenye kijiti juu, ikionesha msimulizi huyo akieleza hadithi yake kwa msisimko.