Farasi Anayekimbia juu ya Mbayuwayu
Radio China Kimataifa


Sanamu hiyo ilitengenezwa kwa shaba nyeusi, na ina kimo cha sentimita 34.5, urefu wa sentimita 45 na upana wa sentimita 10. Ni sanamu iliyotengenezwa katika Enzi ya Han Mashariki (25-220), na ilifukuliwa mkoani Gansu, hivi sasa inahifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Mkoa wa Gansu.

Farasi walikuwa ni kama chombo muhimu vitani, na alama ya heshima ya taifa na nguvu za nchi. Sanamu za farasi za Enzi ya Han ziligunduliwa, lakini iliyoshangaza ni sanamu hiyo.

Farasi huyo anakimbia shoti kichwa juu na miguu mitatu hewani na mguu mmoja tu uko juu ya bawa la mbayuwayu. Misuli inaonesha afya na nguvu za farasi, uzito wote wa farasi uko kwenye bawa la mbayuwayu.

Farasi aliyekimbia ni sanamu adimu kati ya sanamu za kale.