Vivuli vya Picha Zilizotengenezwa kwa Ngozi (1)
中国国际广播电台
 

      Mchezo wa vivuli vya picha zilizotengenezwa kwa ngozi ni aina moja ya michezo ya sanaa inayopenswa na Wachina, mchezo huo umeenea zaidi katika sehemu ya kaskazini magharibi ya China.

Mchezo huo ulikuwa unachezwa sana katika Enzi ya Ming na Enzi ya Qing (karne ya 14 – 19).

 

Picha za ngozi zinatengenezwa kwa ngozi ya ng'ombe mdogo mweusi, ngozi hiyo huwa laini na si nene wala nyembamba. Baada ya kuondoa manyoya na kukaushwa, ngozi hiyo inaweza kutumiwa kutengeneza picha. Kwanza picha inachorwa kwenye ngozi na kisha inakatwa na kuchongwa kwa mujibu wa picha iliyochorwa, baadaye picha inapigwa pasi baada ya kutiwa rangi ambayo inaweza kupitisha mwangaza. Baada ya picha zote zinazohitajika katika mchezo zinapangwa pamoja. Wakati huo mchezo wa vivuli vya picha zilizotengenezwa kwa ngozi unaweza kuchezwa. Mchezo huo unachezwa kwa vivuli vya picha kwenye pazia, vivuli hivyo vinatokea kutokana na mwangaza wa taa unaokuwa nyuma ya picha.

Kwenye upande wa kushoto wa picha ni mungu wa dini ya Dao, na kwenye upande wa kulia ni picha ya Mencius.

 

Mchezo huo unachezwa na huku wachezaji wanaimba kwa sauti ya juu. Kila sehemu ya picha, miguu, mikono, kichwa inaweza kucheza. Ni mchezo unaowavutia sana wenyeji.

Michezo ya vivuli vya picha zilizotengenezwa kwa ngozi huonesha hadithi za historia.