Vitu vya Udongo vya Kuchezea Watoto (1)
中国国际广播电台
 

   Mkoani Henan kuna mila ya kutengeneza vitu vya udongo vya kuchezea watoto. Vitu hivyo huwa ni “kima anayejishika magoti”, “kima mwenye sura ya mtu”, “kima anayempakata mtoto wake”, n.k.

  Vitu hivyo sivyo tena vitu vya kuchezea watoto, bali ni aina moja ya sanaa kutokana na historia ndefu.

Vitu hivyo hufinyangwa kwa udongo, kwenye mgondo au chini kuna kitundu ambacho kikipulizwa kinaweza kutoa sauti. Kima huyo amefinyangwa kwa kupiga chuku, anaonekana kama kima na pia kama binadamu mwenye uso wa mviringo, macho ya duara kama gololi.