Tiara
中国国际广播电台
 

      Tiara ni moja ya vitu vinavyotumiwa na watu. Kurusha tiara pia kunamaanisha kufukuza “kisirani”. Kurusha tiara licha ya kuweza kujifurahisha, pia inaweza kujenga afya, na mchezo huo unaenea zaidi katika sehemu za Weifang, Beijing, Tianjin na Nantong mkoani Jiangsu.

Mkoa wa Shangdong una historia ndefu ya kuchora picha kwenye tiara kama picha za mwaka mpya. Mchezo wa kurusha tiara unachezwa sana katika miji ya Weifang mkoani Shandong, Beijing na Tianjin na mji wa Nantong mkoani Jiangsu.

Uchoraji wa picha kwenye tiara mjini Weifang una historia ya ndefu sana. Picha za huko zina mtindo wazi wa kienyeji.

     Tiara za Beijing zina historia ya miaka 300, tiara za Beijing hutengenezwa kwa umbo la ndege na popo.

Katika picha ni tiara ya ndege mbayuwayu wawili, mmoja wa rangi ya buluu, na mwingine wa rangi nyekundu, ikionesha “mume na mke wanashindana kuruka juu”.