Opera ya Nuo
中国国际广播电台
 

    Opera ya Nuo ina historia ndefu. Opera hiyo ilianzia kufanya matambiko, na ilipokuwa katika Enzi ya Shang (1600 K.K.-1046 K.K.) ilikuwa ni aina ya kufukuza mashetani.

Wachezaji wa opera hiyo huvaa vinyago usoni wakiiga mashetani wa aina mbalimbali.

Katika sehemu ya kaskazini ya mkoa wa Guizhou mpaka sasa bado opera hiyo inachezwa. Wachezaji huwa kiasi cha mia moja wakivaa vinyago vya aina mbalimbali.

Vinyago huchongwa kwa mbao, ambavyo huchongwa kwa sura za kutisha, baadhi vinyago vina pembe, baadhi vina meno marefu, baadhi vina midomo mikubwa, na baadhi macho yanajitokeza sana na nyusi nene nyeusi, vinyago hivyo vinatisha kwa sura.