Picha ya Kuchongwa ya Mwaka Mpya
中国国际广播电台
 

    Picha ya kuchongwa ya mwaka mpya ina historia ndefu.

Picha ya kuchongwa ilianzia Enzi ya Song (960-1297), wasanii walichonga picha kwenye mbao kisha walichapisha, hivyo picha nyingi zilianza kuchapwa na kuuzwa katika enzi hiyo.

Kuanzia Enzi ya Song picha za kuchongwa za mwaka mpya licha ya kuonesha picha za aina mbalimbali za miungu pia zilianza kuonesha matumaini mema ya wakulima.

Picha za kuchongwa za mwaka mpya zilipamba moto katika Enzi ya Qing (1368-1911). Picha kama “mavuno mazuri”, “Ng'ombe alima katika majira ya Spring” n.k. zote ni picha zinazowavutia watu hadi leo. Wachoraji mashuhuri wa picha za kuchongwa za mwaka mpya pia walitokea wengi.