Utarizi wa Kabila la Wamiao
中国国际广播电台
 

      Katika mkoa wa Guizhou wanaishi Wamiao wengi, watu hao wana mila ya kutarizi mapambo kwenye nguo. Vitu wanavyovitarizi huwa ni dragoni, ndege, samaki, maua, vipepeo na tandu.

  Pichani ni aproni iliyotariziwa kwa vipepeo, tandu kwa nyuzi za rangi mbalimbali.

Pambo linalotariziwa kwenye nguo mara nyingi huwa mtu anayepanda dragoni, ikionesha ujasiri na ushupavu wa Wamiao. Kadhalika, pia kuna picha za tarizi za swala, na wanyama wa aina nyingi.