Mfuko wa Kiunoni
中国国际广播电台
 

 Mfuko wa kiunoni ni aina moja ya pambo kwenye kiuno, maumbo ya mfuko yalikuwa ni ya aina mbalimbali, kama duara, mraba, ya mstatili n.k. Picha za vitu vinavyoshonwa kwenye mfuko huo huwa ni maua, ndege na wanyama, ambavyo vinaonesha matumaini mema ya mtu aliyeshona.

Michoro kwenye mikoba pia huanbatana na maneno yakimaanisha matumaini mema na mustakbali mzuri kwa watu wanaotumia mikoba hiyo

Pichani, mfuko huo una umbo la tunguri, na kwenye shindo ya tunguri hilo kuna mashuke ya dhahabu, na kwenye mbele na nyuma kuna maneno “Uwe mnyekekevu wakati wote”.