Vyombo vya Kauri (4)
中国国际广播电台
 

   Vyombo vya Kauri Vyenye Michoro ya Rangi ya Buluu vilikuwa maarufu katika Enzi ya Yuan (1206-1368).

Katika enzi hiyo kulikuwa na matanuri mengi ya kuchomea vyombo hivyo. Vyombo vya kauri vilivyochomwa vizuri vilikuwa hutolewa kwa ajili ya wafalme, na vilikuwa havikuchomwa vizuri huuzwa miongoni mwa raia.

Katika enzi hiyo matanuri yalitapakaa karibu kila mahali nchini China. Michoro kwenye vyombo vya kauri ni ya aina nyingi. Baadhi inaonesha mandhari ya mito na milima, mila na desturi, maua na ndege, matunda na mboga na watu katika riwaya.

 Pichani, ni bakuli lenye michoro ya buluu. Katikati ya bakuli ni mtu mwenye upanga aliyepanda farasi, ingawa picha hiyo imechorwa kwa mistari michache lakini inaonekana kama ya kweli.