Mapango ya Longmen

中国国际广播电台
 

   Mapango ya Longmen yako mkoani Henan, nje ya Mji wa Luoyang kwa kilomita 12.5. Mapango hayo yalichongwa kwenye magenge ya Longmen, mahali penye mandhari nzuri ya kuvutia watalii kwa milima na mito.

  Mapango kwenye magenge ya Longmen yalianza kuchongwa katika Enzi ya Wei Kaskazini wakati wa utawala wa mfalme Xiaowendi (471-477), na yaliendelea kuchongwa katika muda wa miaka 400, mpaka sasa yamekuwepo kwa miaka 1500. mapango hayo yalichongwa kwa kilomita moja kutoka kusini hadi kaskazini, mapango yaliyopo sasa yamekuwepo kwa zaidi ya 1300, mawe yenye maandishi zaidi 3600 na sanamu za Buddha 97000. kati ya mapango hayo kwa mapango ya Binyangzhong, Fengxiansi na Guyangdong.

Pango la Binyangdong lilianza kuchongwa katika Enzi ya Wei Kaskazini (386-512), na kukamilika baada ya miaka 24. ndani ya pango hilo kuna sanamu 11 za Buddha, na kati ya sanamu hizo sanamu ya mwanzilishi wa Dini ya Buddha Sakyamuni ni kubwa zaidi.

Pango la Fengxiansi ni kubwa kuliko mapango yote, ni pango lililochongwa katika Enzi ya Tang (618-904). Pango hilo lina mita 30 kwa upana na urefu. Ndani ya pango hilo sanamu moja ina urefu wa mita 17, macho yake yanangalia na wanaoangalia sanamu hiyo kutoka chini.

Pango la Guyang ni pango lililochongwa zamani zaidi. Ndani ya pango hilo kuna shubaka nyingi ambazo zilichongwa majina ya watu waliochonga na tarehe mwezi na mwaka pamoja na maneno machache ya sababu ya kuchonga shubaka.

Licha ya sanamu, ndani ya mapango pia kuna maandishi na vitu kuhusu dini, uchoraji, muziki, dawa, mapambo ya mavazi. Kwa hiyo mapango hayo ni kama makumbusho ya historia ndefu.

Mapango ya Longmen yaliorodheshwa kwenye kumbukumbu ya urithi wa dunia katika tarehe 30 Novemba, mwaka 2000.