s

Mapango ya Yungang

中国国际广播电台
 

       Mapango ya Yungang yako mkoani Shanxi, karibu na mji wa Datong kwa kilomita 16. mapango hayo yalianza kuchongwa mwaka 453. Kati ya hayo ni 45 tu yaoiyobaki hadi sasa, kuna sanamu zaidi ya 51000, na kati ya sanamu hizo iliyo kubwa ina urefu wa mita 17, na iliyo ndogo ina urefu wa sentimita kadhaa. Mapango hayo yenye sanamu yalichongwa katika miaka mingi iliyopita tokea enzi za Qin na Han (221 K.K.-220) hadi enzi za Sui na Tang (581-907), ni ghala ya usanii wa sanamu za kuchongwa duniani.

  Kutokana na kuwa mapango hayo yalichongwa katika enzi nyingi za kifalme nchini China, sanamu ndani ya mapango hayo ni tofauti katika sanaa, ambazo zimeonesha wazi mitindo tofauti katika enzi tofauti.

Sanamu ndani ya mapango hayo pia zimerikodi jinsi usanii wa dini ya Buddha ya India ulivyoelekea hadi kuwa usanii wa dini ya Buddha ya China.

Usanii katika mapango ya Yungang ni mwanzo wa usanii wa Kichina. Katika mapango yaliyochongwa katika kipindi cha mwisho, sanamu zimekuwa za mtindo wa Kichina halisi.

Mwezi Desemba mwaka 2001 mapango ya Yungang yameorotheshwa katika urithi wa Dunia. Kamati ya Urithi wa Dunia ilitathmini mapango hayo ikisema kuwa mapango hayo yamewakilisha mapango ya Dini ya Buddha kati ya karne ya 5 hadi 6.